Na. John Mapepele

Tamasha la Muziki la Serengeti leo Machi 13, 2022 linaingia katika siku yake ya pili na ya mwisho katika  viwanja wa Chinangali  jijini Dodoma baada ya kazi nzuri ya jana huku  msanii nguli Harmonize kuwa miongoni mwa wasanii wataopanda jukwaani.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka wasanii waliopata fursa kushiriki katika tamasha hili kutoa burudani kabambe ili kuonyesha vipaji vyao na kuitangaza Tanzania.

Wasanii waliopanda jana waliwapagawisha mamia ya  wapenzi waliofurika kuwaburudisha kutokana na umahiri wao wa kutumbuiza, huku wengine wakifanya kolabo kama AY na  Mbunge wa Muheza na Msanii Mkongwe Mwana FA na kuwa miongoni mwa vivutio katika tamasha hili.

Kundi la wasanii machachali na  chipukizi wataungana na wakongwe  ambao watahitimisha tamasha la mwaka huu leo Machi 13, 2022 kwa kiingilio cha  shilingi 3000 getini.

Mbali na wasanii wengi watakao burudisha leo Ma Dj wakongwe wanatarajia kutawala jukwaa kwa vionjo vyao.

Kutokana na uratibu nzuri wa tamasha hili ambalo limeratibiwa na Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana  na wadau kumekuwa na shauku kubwa kwa Wasanii mbalimbali kufanya vizuri ili waweze kuinua  viwango vyao.

Jana wakati  Wasanii wakitumbuiza Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu. Mhe Kassim Majaliwa ilitoa msimamo wa kuendelea kuandaa na kuboresha tamasha ili kuendelea kutumia sanaa kuitangaza Tanzania kimataifa.
 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...