Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amemkabidhi zawadi ya mfano wa meli mwanamuziki maarufu  Duniani mwenye asili ya Lebanoni Maher Zain kutoka nchini Sweden anayejulikana kwa Nyimbo za Kaswida, kama sehemu ya kuhamasisha utalii hapa nchini.

Waziri Mchengerwa amemkabidhi zawadi hiyo  katika tamasha la siku moja lililofanyika usiku wa Machi 12 jijini Dar es Salaam, maalum kwa ajili ya kuwezesha ununuzi wa  vyombo vya usafiri na kukuza kipato kwa walemavu wasio ona  wanaolelewa katika kituo cha Vimdat kilichoko Kisemvule jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mamia ya mashabiki wake waliofurika kuburidika na nyimbo zake kabla ya kuhitimisha tamasha hilo, mwanamuziki huyo maarufu wa Qaswida duniani aliyevalia tisheti yenye maneno (Tanzania Unforgettable) amesema uwepo wake Tanzania ni jambo asiloweza kulisahau Maishani mwake kutokana na uzuri wa Tanzania na ukarimu wa watu wake.

“Naishukuru Serikali ya Tanzania na ninakupongeza Mheshimiwa Waziri kukuona hapa na wewe umekuja kuburudika na nyimbo zangu kweli Tanzania siyo ya kusahulika” alisme Maher

Akizungumza kwa niaba ya waandaji wa tamasha hilo Mwenyekiti msaidizi Yousra Alnahd amesema tamasha hilo lililopewa jina la Maher Zain in Tanzania pamoja na mapato ya tamasha hilo kulenga ununuzi wa vyombo vya usafiri kwa ajili ya kituo hicho, pia waandaji walilenga kuitangaza utalii kama sehemu ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu katika kuitangaza Tanzania na vivutio vyake.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...