Na Khadija Kalili, Kibaha

Balozi wa Korea nchini Kim Sun Pyo amezindua rasmi Chumba Cha Kutakasia Vifaa Tiba kilichopo katika Hospital ya Rufaa ya Tumbi iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Balozi Pyo alisema kuwa uzinduzi huo umefanyika mara baada ya kumalizika kwa ukarabati wa majengo hayo uliotokana na ufadhili wa Taasisi ya Kikorea inayofahamika kwa jina la Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH).

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Amani Malima alisema kuwa Hospital hiyo imeongeza wigo wa utoaji wa huduma za Afya ambapo hivi sasa inahudumia wagonjwa wengi zaidi wanaofika Hospitalini hapo baada ya kupata Rufaa ,wasio na wenye Rufaa kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Pwani.

Mganga Mfawidhi Malima aliongeza kwa kusema kuwa Hospital hiyo wanapokea majeruhi wengi wa ajali kwa kuwa wako pembezoni mwa barabara kubwa iendayo Mikoani.

"Kutokana na ongezeko la uhitaji wa vifaa tiba safi na salama vilivyotakaswa kwa kufuata sheria na taratibu za kitabibu , ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa ambao ni majeruhi wahitaji wa huduma za upasuaji huduma za kusafisha vidonda na huduma nyingine zinazohusiana na hizo, Uongozi wa Hospitali ulifikia hatua ya kuona umuhimu wa kuwa na Chumba Cha Kutakasia Vifaa ambacho kitarahisisha upatikanaji wa huduma za utakasaji wa vifaa kwa wagonjwa ili kupunguza maambukizi"alisema

Malima alisema kuwa mradi mzima wa kukarabati Chumba Cha Kutakasia Vifaa umegharimu kiasi cha Mil 232,560,000 huku vifaa na ukarabati wa vyumba vya Kutakasia ukigharimu kiasi cha Mil.52,630,000 na ununuzi wa mashine pamoja na kusimika ni Mi.179,930,000.


Wakati huohuo Mganga Mkuu w Mkoa wa Pwani Dkt. Gunini Kamba alisema wamemtembeza Balozi Pyo kwenye jengo la watoto njiti ambapo kwa siku hupokea watoto kati ya 30 hadi 40 ambao wanazaliwa kabla ya umri wa miezi sahihi ya kuzaliwa.

"Hapo awali hatukuwa na majengo haya ambapo baada ya ukarabati mkubwa uliofanyika sasa hali ya kutunza watoto hawa ambao almaarufu kama njiti umekuwa rahisi na salama kwa mama na mtoto"alisema Dkt. Gunini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...