Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete akitoa maelekezo kwa Meneja wa Bandari ya Ziwa Viktoria, wakati alipotembelea Bandari ya Kemondo, Mkoani Kagera.Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete (katikati), pamoja na Viongozi mwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mzani uliojengwa katika bandari ya Kemondo, Mkoani Kagera.Gari la mizigo likipima katika mzani mpya uliojengwa katika Bandari ya Kemondo Mkoani Kagera.


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,-Uchukuzi Atupele Mwakibete akimsikiliza Karani kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Dalila Shakiru, Wakati akimweleza namna hatua za upimaji zinavyofanyika, mara baada ya Naibu Waziri huyo kuzindua rasmi matumizi ya mzani huo katika bandari ya Kemondo, Mkoani Kagera.


Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Viktoria, Vicent Stephen akifafanua kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete kuhusu maboresho ya bandari ya Bukoba, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Bandari hiyo Mkoani Kagera.Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Ziwa Viktoria, Vicent Stephen (wa tatu kulia) wakati alipotembelea Bandari ya Bukoba, Mkoani Kagera.PICHA NA WUU

……………………………………………….

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa mzani katika bandari ya Kemondo mkoani Kagera ni miongoni mwa mwendelezo wa njia zinazotumika kupata idadi halisi ya mzigo unaoingia na kutoka bandarini hapo ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.

Amezungumza hayo mkoani Kagera, wakati akifungua rasmi mzani huo ambao umekamilika kujengwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 34.

Naibu Waziri huyo amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejikita katika kukusanya mapato hivyo itaendelea kuwekeza fedha kwenye miudombinu ili kuziimarisha kimapato na kuongeza tija.

“Kumekuwa na mianya mingi ya upotevu wa mapato katika maeneo mbalimbali hivyo tunaimarisha miuondombinu sambamba na mifumo hivyo nina Imani uwepo wa mzani huu tutajua sasa mzigo unaoingia na kutoka na kudhibiti mapato”, amesema Naibu Waziri Mwakibete.

Naibu Waziri Mwakibete ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kuharakisha taratibu za manunuzi kwa ajili ya mradi upanuzi wa bandari ya Bukoba, Kemondo na Mwanza ili kwenda sambamba na ukamilikaji wa meli ya MV Mwanza.

Aidha, Naibu Waziri Mwakibete ameongeza kuwa pamoja na utekelezaji wa miradi hiyo Mamlaka ihakikishe miradi yote inazingatia thamani ya fedha ili kukamilika kwa ubora.

Naye Kaimu Menenja wa Bandari za Ziwa Viktoria, Vicent Stephen, amesema maboresho yaliyofanywa kwa bandari ya Kemondo yameongeza huduma ya shehena kufikia tani 9,652 kwa mwaka 2022 ikilinganisha na tani 3,436 kwa mwaka 2021 na kupandisha mapato kufikia milioni 165 kwa mwaka 2022 kulinganisha na 108 kwa mwaka 2021.

Stephen ameongeza kuwa kwa mwaka 2021/22 Mamlaka imetenga bilioni 8 kwa ajili ya kuboresha gati, jengo la abiria, uzio na miuondombinu mingine katika bandari ya Kemondo ili kuruhusu meli ya MV Mwanza kapakia na kupakua mizigo itakapoanza huduma.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete yuko mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya sekta inayoendelea mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...