Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka waendesha pikipiki maarufu bodaboda kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani kwa lengo la kujiepusha na ajali zinazosababisha vifo na majeruhi.

IGP Sirro amesema hayo akiwa Buseresere mkoani Geita wakati  aliposimamisha msafara wake kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ambapo IGP Sirro amesema kuwa, kutokana na jitihada zinazofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amewapatia wakazi wa eneo hilo gari moja itakayosaidia kutoa huduma za kipolisi kwa haraka.

Aidha, IGP Sirro ameahidi kutoa kiasi cha shilingi laki tano kwa mwananchi yeyote atakayefichua mhalifu anayetumia silaha ya moto.

Naye kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza SACP Ramadhani Ng’anzi amesema kuwa, Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limeendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoa wa Geita kwa kufanya Operesheni za pamoja za kudhibiti uhalifu na wahalifu.




 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...