TAASISI ya Ukaguzi wa hesabu za ndani (IIA) imezindua nembo mpya pamoja na tovuti (Website) kwaajili ya kuelimisha Umma juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na taasisi hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Nembo mpya, Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Jenisia Mpango amesema kuwa uzinduzi wa nembo na tovuti ya taasisi hiyo ni kuendana na mabadiliko yanayojitokeza utekelezaji wa majukumu ya utekelezaji wa ukaguzi wa hesabu za ndani.
Amesema ukaguzi wa hesabu za ndani unakua kama mwili wa binadamu unavyokuwa hii ndio imepekea Ukaguzi wa hesabu za ndani uendane na mabadiliko hayo.
"Kwahiyo tumekuwa na hiyo nembo pamoja na tovuti ili kuendana na mabadiliko, kwasababu hiyo nembo inaongea kulingana na mabadiliko yanayotokea." Amesema Jenisia
Amesema nembo ya awali imekaa kwa zaidi ya miaka 75 ambayo ni sawa na umri wa mtu hivyo ndio sababu ya kuamua kubadilisha nembo hiyo ili kuwa na nembo mpya kuweza kuonesha uhalisia wa mabadiliko katika mazingira, mabadiliko ya teknolojia na utendaji wa hesabu za ndani.
"Hii imeonesha jinsi ambavyo ukaguzi wa hesabu za ndani ulivyo mhimu katika maendeleo ya kila taasisi hasa hapa nchini pamoja na Zanzibar." Amesema Jenisia
Amesema maendeleo yahawezi kwenda bila kujitazama na kujitathmini hivyo Mkaguzi wa hesabu za ndani yupo kwaajili ya kuangalia sheria kama zinafuatwa pamoja na kuangalia matarajio ya kila taasisi yanatekelezwa kama yalivyo pangiliwa.
Jenisia amesema kuwa taasisi haiwezi kuendelea bila kuwa na mkaguzi wa hesabu za ndani ambaye atakuwa anaonesha wazi wazi jinsi ambavyo malengo yanafuatiliwa katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali.
Kwa Upande wake Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa hesabu za ndani (IIA) Tanzania, CPA Zelina Njeza amesema uzinduzi wa nembo mpya ya taasisi yao ni mhimu katika historia ya ukaguzi wa hesabu za ndani hapa nchini.
Amesema kuwa muonekano mpya wa nembo mpya (logo) umelenga katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa wakaguzi wa hesabu za ndani pamoja na wasau wanaofanyanao kazi.
"Tumezindua nembo yetu mpya baada ya kufanya utafiti ili kuhakikisha tunahudumia watu wanaoendana na mabadiliko ya teknolojia." Amesema Zelina
Amesema kuwa changamoto katika taasisi hiyo ndizo sinazosababisha kuendelea kuleta mabadiliko hivyo elimu ya mkaguzi wa ndani inaendelea kutolewa katika taasisi mbalimbali.
Amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu ili wafanyakazi wa taasisi waweze kuwatumia wakaguzi wa ndani.
Mkaguzi Mkuu wa hesabu za ndani kutoka zanzibar, Fatma Khamis Mohamed amesema kuwa wakaguzi wa hesabu za ndani ni kama jicho la Serikali kwa sababu katibu mkuu na watendaji wengine hawawezi kufatilia utendaji wa taasisi nyingine.
Nembo ya taasisi ya IIA iliyozinduliwa leo inarangi mbili ambazo ni kijani ikiwakilisha Ardhi yetu na rangi ya blue ikiwakilisha Maji huku ikiwa imegawanyika katika vipande sita ambavyo huwakilisha mabara Sita ya dunia.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Jenisia Mpango na Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa hesabu za ndani (IIA) Tanzania, CPA Zelina Njeza wakiungua pazia kuashiria uzinduzi wa Nembo (Logo) ya Taasisi ya Ukaguzi wa hesabu za ndani (IIA) leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Jenisia Mpango akizungumza wakati wa uzinduzi wa Nembo (Logo) ya Taasisi ya Ukaguzi wa hesabu za ndani (IIA) leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.
Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa hesabu za ndani (IIA) Tanzania, CPA Zelina Njeza akizungumza wakati wa uzinduzi wa Nembo (Logo) ya Taasisi ya Ukaguzi wa hesabu za ndani (IIA) leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Jenisia Mpango katikati akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Nembo (Logo) ya Taasisi ya Ukaguzi wa hesabu za ndani (IIA) leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Jenisia Mpango katikati akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Nembo (Logo) ya Taasisi ya Ukaguzi wa hesabu za ndani (IIA) leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau waliohudhulia uzinduzi wa Nembo (Logo) ya Taasisi ya Ukaguzi wa hesabu za ndani (IIA) leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...