Na WMJJWM Arusha

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju ameiasa jamii kupambana na vitendo vya ukatili hasa dhidi ya Wanawake ili kutorudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau za kuleta Usawa wa kijinsia.

Ameyasema hayo mkoani Arusha katika Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililowakutanisha Wanawake na wadau wengine kujadili changamoto zinazowakabili Wanawake na Ustawi wao.

Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kusimama katika kupambana na kupinga Mila hasi za kumnyima mwanamke haki na kumkandamiza katika kupata fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii ili kumuwezesha mwanamke kuwa na uwezo wa kutatua changamoto zinazomkabili.

Aidha ameitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kusaidia kubadili fikra kwenye jamii ya namna wanavyomthamini na kumshirikisha mwanamke katika masuala mbalimbali hasa yanayohusu maamuzi ndani ya familia na jamii.

Pia ameitaka jamii na wadau mbalimbali kuendelea kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika vyombo husika ili kusaidia juhudi za Serikali na wadau kupambana na vitendo vya ukatili ili kuwa na Tanzania isiyo na vitendo vya ukatili.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya uendeshaji Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Rosemarie Mwaipopo amesema Taasisi itaendelea kusimamia utekelezaji wa afua mbalimbali za kuhakikisha wanawake wanawezeshwa ili kuhakikisha wanapata fursa sawa katika Sekta mbalimbali.

Naye Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt Bakari George amesema lengo la Kongamano hilo ni kuwakutisha Wanawake na Makundi mengine na kuhakikisha kuwa Wanawake wanapata fursa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashiriki Peter Mathuki amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Usawa wa kijinsia unazingatiwa katika kipindi chakecha uongozi hasa mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto hivyo ameihakikishia Wizara kuendelea kushirikiana nayo ili kuunga mkono mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili.

Akizungumza katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Shirika la Legal Service Facility (LSF) Lulu Ng'wanakilala amesema Shirika lake litaendelea kusaidia Wanawake kupata haki zao katika masuala ya kisheria na kusema kuwa kati ya matukio kumi matukio manne yanayoripotiwa katika takwimu za Shirika hilo matukio hayo ni ya unyanyasaji wa Kijinsia ikiwa ni sawa na asilimia 26.5.

Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju amezindua Programu ya mafunzo kwa Wasichana na daftari la kieletroniki la wajasiriamali na matokeo ya uzinduzi huu ni kuwawezesha wasichana kupata mafunzo ya Uongozi na kuwawezesha wajasirimali Machinga kwa kuwatambua na kuwasajili kwa lengo la kuwaunganisha katika fursa mbalimbali.

Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Shirika la Legal Service Facility (LSF) imeandaa Kongamano la Kitaifa la Wanawake lenye lengo la kuwakutanisha Wanawake na wadau wengine katika kujadili changamoto zinazowakabili Wanawake na Ustawi wao.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizindua Programu ya mafunzo kwa Wasichana na daftari la kieletroniki la wajasiriamali na matokeo ya uzinduzi huu ni kuwawezesha wasichana kupata mafunzo ya Uongozi na kuwawezesha wajasirimali Machinga kwa kuwatambua na kuwasajili kwa lengo la kuwaunganisha katika fursa mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...