Adeladius Makwega-DODOMA

Wangindo ni miongoni mwa makabila madogo katika jamii ya Watanzania ambalo limetanyika mno kama nilivyokudokeza katika matini yangu ya kwanza, huku likiwa na makabila mengi watani wake.

Neno Utani wa Kindingo ni KUTANILA.

Miongomi mwa vita hatari mno walivyopigana ni VITA vya MACHONDA walipigana na Wangoni, vita hivi wangindo walitumia mishale na mikuki ambayo ilikuwa na sumu, jambo hilo liliwasumbua mno Wangoni waliokuwa mabingwa wa vita lakini wagombanao ndiyo wapatanao na mwisho wa siku walikuja kuwa watani huku wakioleana( Hapo kumbuka wale Wangindo wa Ilonga –Ulanga Morogoro).

Wangindo wakawa watani hata makabila makubwa ambayo yalikuwa na nguvu kubwa kama Wayao, Wasangu, Wanyakyusa na Wahehe. Huku ikiaminika kuwa Wangindo ni watani na makabila karibu yote yale ya Kusini mwa Tanzania.

Utani huo unaonekana hata kwa Wanyamwezi, Wanyamwange, Warufiji (Wandengereko), Wamakua, Wasangu, Wambunga na Wafipa.

Wangindo ni watani na wanyamwezi si kwa sababu ya vita bali kutokana na biashara ya utumwa na ujio wa Waarabu. Mwarabu alikuwa na kambi zake kubwa za kuwakusanya watumwa na mizigo yao huko Tabora na Liwale.

Wakati wakielekea bahari ndipo walipokutana na Wangindo na ndiyo kusema Wayao na Wanyamwezi walioshirikiana mno na Waarabu wakawazoea Wangindo kwani wakiwa njiani walikuwa wakila vyakula vinavyolimwa na Wangindo na pengine bila ya kuomba baada ya Masurufu (posho)yao kumalizika, jambo hilo likajenga utani baina yao.

Kumekuwa na hoja ya ujio wa Wanyamwezi kulima karanga huko Liwale na Nachingwea kwani Mjerumani alipoanzisha kilimo hicho Wanyamwezi walitumiwa kama vibarua, kweli jambo hilo lilisaidia kujenga udugu baina ya Wangindo na Wanyamwezi.

Kwai ndani ya mashamba ya karanga Mjerumani hakuruhusu kulima matunda kama mapapai na ndizo hivyo Wanyamwezi waliwatembelea Wangindo na kupata matunda hayo hapo ujirani ukaanza.

Katika kabila hil wanaruhusu mtoto wa mjomba kumuoa mtoto wa shangazi. Katika kabila hili kijana wa kiume huwa na wajibu wa kulipa mahari na kabala ya harusi binti huyu uchumbiwa

Katika familia walikuwa wakichumbiwa hata kabla hawajapevuka (KIGORI-NNHWENJA) jambo hilo lilimgharimu mchumba wa kiume (mposaji) kwenda kuwajibika kukaa huko ukweni tarajiwa hadi binti huyo kupevuka.

Kijana huyu alikaa hapo huku akifanya kazi mbalimbali za ukweni naye binti akishapevuka aliwekwa ndani huku akifanya kazi ndogo ndogo kama kusaga nafaka, kupika ndani ya nyumba hii tu akila na kulala kwa kipindi fulani. Hapa hawa waliopasana walikuwa hawakai chumba kimoja kila mmoja alikuwa na sehemu yake.

Baada ya hapo akiwa MWALI ndipo harusi hufanyika. Kwa hiyo kuona kwa mtoto wa mjomba na shangazi ilikuwa ni jambo zuri hata kama mtoto wa mjomba anaposa kwa shangazi yake anakwenda kufanya kazi kwa shangazi yake na hata mahari inakuwa si jambo kubwa inakuwa ya kawaida kwani ndugu kwa ndugu wanafunga ndoa.

Pia kulikuwa na hoja ya ugumu wa kuvunjika kwa ndoa baina ya mtoto mjomba na shangazi kwani kwani mazungumzo ya pande zote mbili yanafanyika kwa wepesi. Hata watoto wanaozaliwa wanabaki kuwa ni mali ya jamii ile ile hawezi kupotea kwenda kuwa watoto wa ukoo mwingine wa mbali.

Jambo hili kwasasa linakumbwa na upinzani kwa hoja mbili, kwanza kuwa si vizuri kuoana baina ya mtoto wa mjomba na shangazi kwani hao ni ndugu kabisa huku kukiwa na hoja pili kwa sasa jamii zetu zinazungukwa na watu wengi ni vizuri kujichanganya na watu wengine ili kuondoa magonjwa ya vinasaba kama wakioana watu wanaokuwa na nasaba moja.

Mwanakwetu kwa leo naishia hapo kwa ndugu zangu Wangindo.

Nakukumbusha kuwa katika matini ijayo nitawataza ndugu zetu Wanyakyusa.


Nakutakia siku njema.


makwadeladius@gmail.com

0717649257 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...