Na Pamela Mollel,Arusha
Jamii imeshauriwa kutumia kwa wingi Mchicha lishe wa Akeri uliofanyiwa utafiti wa kina na Taasisi ya utafiti wa kilimo(TARI-Tengeru)na kugundulika kuwa na virutubisho vingi hasa madini ya Zinki ili kuondokana na tatizo la udumavu
" Kwa wanaume wenye changamoto ya tendo la ndoa mchicha huu unasaidia kuimarisha majukumu yao ikiwemo kuboresha mfumo wa uzazi"
Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari jijini Arusha,waliopatiwa mafunzo na Tume yaTaifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH)Mtafiti Mwandamizi Emmanuel Lasway kutoka TARI alisema Mchicha huo umepewa kipaumbele kwa sababu unaweza kutumia majani na mbegu
Alisema kuwa kwa sasa wanashauri jamii hasa wanaume kutumia nafaka ya Mchicha wa Akeri kutokana na namna ambavyo umefanyiwa utafiti na kugundulika unaprotini 14.5%huku ukiwa ni chanzo bora cha vitamini A,B,Zinki,madini ya chokaa,chumvi na folikasidi
Mtafiti huyo aliongeza kuwa Mchicha huo wa maajabu huvunwa shambani na kisha mbegu zake husagwa na kuchanganya kwenye vyakula ili kuongeza virutubisho
"Unga wa Mchicha huchanganywa kwenye unga waugali,vitafunwa,uji,shurubati na vyakula vingine ili kuongeza virutubisho "alisema Lasway
Hata hivyo Mchicha huu unatajwa kuwa na protini nyingi zaidi ya mahindi na ngano
"Mchicha lishe huu unachangia kiasi cha 50-102%folikasidi ukilinganisha na mahindi 15-46%na ngano 20-51%"alisema Lasway
Pia Mchicha huu unatajwa kuwa ni mzuri kwa ukuaji watoto na wajawazito
Ukosefu wa kula mboga na matunda husababisha ukosefu wa damu,udumavu na uoni hafifu
Uzalishaji wa mbegu ulianza rasmi 2018 ambapo kwa sasa mbegu hizo hupatikana kituo cha TARI Tengeru na wakala wa mbegu (ASA)
Mafunzo ya siku 4 ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari yaliyofadhiliwa na COSTECH yalilenga kuwajengea uwezo waandishi kuandika habari za Sayansi na Teknolojia
Picha ikionesha Mchicha wa Akeri uliofanyiwa utafiti wa kina
Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI-Tengeru Emmanuel Lasway akielezea maajabu ya Mchicha huo wa AkeriMbegu za Mchicha wa Akeri kabla haujasagwa na kuwa unga,unga huu unatajwa kuwa na virutubisho vingi kwa afya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...