Na Abdulatif Yunus - Michuzi TV Kagera

Uongozi wa Shule na Wanafunzi wa Josiah Sekondari iliyopo Bukoba Manispaa kwa Kushirikiana na Wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya CRDB wameungana na Wanawake wengine Ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa kupanda miti aina ya Palm Katika Viwanja vya Shule hiyo.

Tukio hilo lililoratibiwa na Shule hiyo ya Wasichana, limehusisha pia upandaji wa Miti mingine ya matunda ikiwemo Parachichi iliyopandwa eneo hilo la Shule lengo likiwa ni kuweka mazingira yao safi, kupamba shule yao sambamba na kuunga mkono Kampeni ya Upandaji Miti aina ya Palm inayoendelea ndani ya Manispaa ya Bukoba Iikisubiriwa kuzinduliwa rasmi.

Awali kabla ya Upandaji miti Wadau mbalimbali wakiwemo Bukoba Tours, Shekhaina Pharmacy, Benki ya CRDB na wengine, wamepata fursa ya kuzungumza na Wasichana hao, baada ya Majadaliano yaliyofanywa na Wanafunzi wenyewe wakati wakiwasilisha mada mbalimbali zenye kuwajenga na kuwakumbusha thamani yao kama watoto wa Kike.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...