Na Pamela Mollel,Arusha

Kamati ya kudumu ya bunge uwekezaji wa mitaji ya umma imepongeza serikali,bodi na menejiment ya uongozi wa Auwsa kwa usimamizi wa mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 520.

Akizungumza katika ziara iliyofanywa na kamati hiyo ya kutembelea na kukagua mradi wa AUWSA wa mabwawa 18 ya kutibu maji , mwenyekiti wa kamati hiyo ambae Ni mbunge wa Ilala Jery Slaa amesema kuwa anaipongeza serikali na bodi ya Auwsa kwa kuwa kazi hiyo imefanyika kwa asilimia 82.

Amesema kuwa anapongeza serikali pamoja na menejiment na uongozi kwa kusimamia mradi huo kwa uadilifu mkubwa kwani kazi Ni nzuri na umeshakwishafikia asilimia 82 ya Utekelezaji na matunda yake yameshaanza kuonekana.

Amewataka wananchi wa Arusha kutunza miundo mbinu hiyo ili kuweza kuleta tija kwa serikali kwa ajili ya kuboresha uchumi wa nchi.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa AUWSA mhandisi Justine Rujomba amesema kuwa anashukuru kwa kamati hiyo kukagua miradi yao na kazi yao Ni kuhakikisha wanatimiza malengo ya mradi huo.

Naye mwenye kiti wa bodi ya Auwsa mhandisi Richard Masika ameeleza kuwa Hadi Sasa Utekelezaji umefikia asilimia 82 na wananchi wameshaanza kuona manufaa yake na kwa Sasa wapo hatua ya pili ya mradi

Kamati ya kudumu ya bunge uwekezaji wa mitaji ya umma wakiongozwa na mwenyekiti wao Jerry Slaa wakikagua miradi ya kuboresha huduma ya maji usafi wa mazingira katika jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Arumeru
Mkurugenzi mtendaji wa AUWSA Mhandisi Justine  Rujomba akitoa maelezo ya mradi kwa kamati ya kudumu ya bunge uwekezaji wa mitaji ya umma
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge uwekezaji wa mitaji ya umma Jerry Slaa akisalimiana na mwenyekiti wa bodi ya AUWSA Mhandisi Richard Masika kulia ni mkurugenzi mtendaji wa AUWSA Mhandisi Justine Rujomba
 

Kulia ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge uwekezaji wa mitaji ya umma Jerry Slaa akiwa na mwenyekiti wa bodi ya AUWSA Mhandisi Richard Masika wakikagua baadhi ya miradi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...