Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akitawalishwa kuwa kiongozi wa wazee wa Mkoa wa Manyara kwa jina Akoo kutoka kwa wazee wa mila wa kabila la Gorowa leo tarehe 16 Machi 2022 wakati alipokutana na kuzungumza na viongozi wa dini na wazee wa mkoa wa Manyara.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na wazee pamoja na viongozi wa dini wa Mkoa wa Manyara katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria kilichopo Babati leo tarehe 16 Machi 2022 alipohitimisha ziara yake mkoani humo.

*************************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 16 Machi 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Manyara, mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Babati mkoani Manyara.

Akisoma risala kwa niaba ya wazee wa mkoa wa Manyara katibu wa Wazee Naomi Kapambala amesema wanafurahishwa na mwenendo wa serikali ya awamu ya sita katika kutatua kero mbalimbali pamoja na kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha ameiomba serikali kukamilisha kujengwa kwa vitengo vyote katika hospitali ya Rufaa ya mkoa pamoja na kuwekwa vifaa tiba ili kupunguza gharama za wananchi wakiwemo wazee kwenda mikoa ya jirani ya Dodoma na Kilimanjaro kufuata huduma za matibabu. Pia Bi. Naomi ameomba kutatuliwa kwa mgogoro wa mpaka uliopo baina ya hifadhi ya taifa ya Tarangire na vijiji vya Gijadabung,ayamango na Gedamar Wilaya ya Babati Vijijini.

Akizungumza na wazee hao pamoja na viongozi wa dini, Makamu wa Rais amewaasa kuendelea kuliombea taifa na wakati wote kutoa ushauri utakaoongza taifa katika amani na mshikamano. Makamu wa Rais amesema baraza ya wazee yanapaswa kutumika ipasavyo mkoani Manyara ili kuendelea kulinda maadili ya chama pamoja na jamii. Amesema wazee wanapaswa kuendeleza mila na desturi za watanzania ili kuwasaidia vijana kuwa wazalendo kwa nchi pamoja na tabia njema.

Halikadhalika, Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema serikali ya awamu ya sita itaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili wazee husasani katika sekta ya afya na mafao. Amewasisitiza watendaji waliopo katika mifuko ya mafao pamoja na hazina kuongeza kasi ya ulipaji wazee mafao yao kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kutoa Trioni 1.2 kwaajili ya ulipaji mafao.

Katika mkutano huo, wazee wa mila wa kabila la Gorowa wamempa uongozi wa kabila hilo kwa jina la Akoo pamoja na uongozi wa wazee wa mkoa wa Manyara Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...