Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Japhet Hasunga akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo mara baada ya Kamati kutembelea na kukagua mradi wa Ujenzi wa Mahakama Jumuishi Temeke na Kinondoni, kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mhakama Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel na kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mheshimiwa Geofrey Pinda
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), chumba cha wakinamama wanachotumia kunyonyeshea katika Mahakama Jumuishi ya Temeke wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Mahakama hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), maeneo mbalimbali katika Mahakama Jumuishi ya Temeke wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Mahakama hiyo
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), maeneo mbalimbali katika Mahakama Jumuishi ya Temeke wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Mahakama hiyo.
PICHA NA OFISI YA BUNGE
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...