*Hospitali ya Aga Khan kuongezewa jengo kwa ajili ya Saratani
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
TASISI ya Aghakan kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la UFARANSA, AFD kuanza mradi mtambuka wa saratani (TCCP) unaolenga kuboresha miundombinu ya matibabu ya saratani nchini.
Akizungumza katika semina iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusiana na mradi wa TCCP wenye lengo la kuwajengea uwezo, mradi Meneja wa mradi huo Daktar Bingwa wa Magonjwa ya saratani wa Taasisi ya Ocean Road Harrison Chuwa amesema kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa yatakayopatikana katika mradi mtambuka wa (TCCP) ni pamoja na kufunga mashine ya ultrasound ya kisasa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road yenye thamani ya Sh. milioni 150 ambayo itahudumia wagonjwa takribani 50 hadi 80 kwa siku.
Amesema katika mradi huo litanunuliwa gari kwa ajili ya kutoa huduma za upimaji wa kansa katika jiji la Dar es Salaam ambapo itarahisisha wananchi kufikiwa na huduma.
Dk.Chuwa amesema mradi huo utajenga jengo katika hospitali ya Aga Khan na watu wenye msamaha wa matibabu watatibiwa katika hospitali hiyo.
Hata hivyo amesema mradi huo unatekelezwa katika Mikoa ya Dar es Salaam pamoja na Mwanza kwa upande wa Mwanza wataweka mashine za kisasa za uchnguzi na matibabu ya magonjwa ya Kansa.
Naye Mtaalamu wa Masuala ya Saratani kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt.Carolyine Swai amesema utumiaji wa tumbaku na pombe kupita kiasi huchangia kwa kiasi kikubwa katika maambukizi ya magonjwa ya saratani na kuwa ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi umekuwa ukitokea mara nyingi kwa wanawake kuliko kwa wanaume, na pia huambukizwa kwa wingi kupitia ngono sisizo salama.
Kwa upande wake David Siso ambae ni meneja Program wa Taasisi ya Ocean Road amefafanua kuwa kupitia Mradi Mtambuka wa Saratani (TCCP) wanatarajia kujenga hospitali ya saratani yenye mashine mbili za kisasa za mionzi ya nje (Linacs) na mashine moja mionzi ya ndani (Brachytherapy) katika Hospitali ya Aga khan Dar es Salaam ambapo ujenzi huo utaanza mwezi Aprili 2022 lengo kuu ikiwa ni kuboresha huduma za saratani Nchini.
Mradi huo unatekelezwa katika wilaya 13 za mikoa ya Dar es salaam na Mwanza ambapo utaweza kusaidia upimaji wa saratani na watakaogundulika kuanza matibabu mara moja kuliko ilivyosasa.
Mwezeshaji wa Aga khan Foundation Brendalinny John akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuwajengea uwezo kuhusiana na mradi mtambuka wa Kansa (TCCP) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi wa Saratani Mtambuka (TCCP) Daktari Bingwa wa Maginjwa wa Saratani wa Taasisi ya Ocean Road Harrison Chuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na magonjwa ya kansa kuwa mradi huo utakwenda kuboresha huduma ya magonjwa hayo,jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Magonjwa ya Saratani wa Taasisi ya Ocean Road Carolyne Swai akiwasilisha mada kwa waandishi habari kuhusiana na magonjwa ya Saratani ,jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja kati ya waandishi wa habari wakiwa wataalam wa mradi mtambuka wa saratani (TCCP) mara baada huhitimishwa kwa mafunzo ,jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...