Kampuni ya kutengeneza simu ya Oppo ambayo ni moja kati ya chapa tano bora duniani, leo imetangaza kuzindua smartphone mpya ambazo ni Oppo A76 na A96 kwa soko lake la Tanzania. Hapo awali, kampuni hii ambayo ina Zaidi ya miaka mitatu kwa hapa Tanzania ilikwa na series A pamoja na reno series.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kuzindua smartphone hizo za A76 na A96 mwishoni mwa wiki, Meneja Mafunzo wa kampuni ya Oppo Tanzania Farida Mwangosi alisema, ‘‘Tunajivunia leo kwa kuzindua simu mpya na ya kisasa ya A76 na A96 huku tukilenga kuhudumia wateja wa kipato cha kati na cha chini kwa bidhaa zenye ubora na unafuuu. Simu hizi ni za kisasa na uhakika, tumeona ni vyema kwa Watanzania wote kuendana na ulimwengu wa kidigitali kwa kutumia simu za smartphone zilizo bora’, alisema Mwagosi huku akiongeza kuwa simu hizi zimekuja na tekinolojia kabambe kukidhi mahitaji ya kila Mtanzania.
Mwangosi aliongeza kuwa Oppo A96 imetengezwa na kuwa na mwanga mzuri na haiwezi kuchuka kirahisi. ‘Simu hii hata ukiwa na mikono michafu kama vile mafuta haichi alama ya vidole na pia ina ram 8 ambazo zinaweza kuzidi mpaka 13 huku ikiwa na memory ya 256GB’.
Aliongeza kuwa Oppo A96 ina uwezo mkubwa wa battery ya 5000mAh na uwezo wa chaji wa 33W na uwezo wa chaji kwa dakika 6o na simu kujaa. ‘Kulingana na teknolojia yake, simu hii ina uwezo wa kutambua jinsi unavyo chaji kwa haraka kwa asilimia 80 na baada ya hapo itaanza kuchaji taratibu hadi utakapoitoa kwenye umeme. Hii inaongeza uwezo wa battery kwani haitaweza kuwa chaji Zaidi ya uwezo wake’, Mwangosi alisema.
Kwa upande wa Oppo A76, inakuja na ram 6+128 lakini inauwezo wq kujiongezea ram 5 juu yani ukawa na ram 11,pia Oppo A96 inakuja na ram 8+256 na inatekinolojia ya kujiongezea ram hadi ram 13 hii inamaana simu hizi mbili zina uwezo wa kujiongezea ram 5 juu ili kumsaidia mteja aendelee kufurahia matumizi ya mtandaoni bila simu kustuck
‘Simu zote hizi zina usalama na uhakika kwa kuwa inauwezo wa kutambua sura na pale inapotambua kuna sura ambayo sio mmliki wa simu yenyewe, basi ina uwezo wa kuzuia taarifa yeyote mpya kuonekana’.
Simu zina waranti ya miaka miwili na kwa betri waranti yake ni miezi sita huku zikipatikana kwa maduka yote ya simu jijini Dar es Salaam lakini pia kwemye wakilishi wa Oppo ambao wapo mikoa ya Morogoro, Dodoma, Arusha, Mwanza, Moshi, Geita, Shinyanga na Tanga pamoja na mikoa mingine.
Kauli mbiu yetu ni Oppo ndio mchongo...oppo vibe na tekinolojia kitofauti.
Meneja Mafunzo wa kampuni ya kutengeneza simu ya Oppo Tanzania Farida Mwangosi (kushoto) akionyesha simu ya smartphone mpya ya Oppo A96 baada ya uzinduzi wake uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Oppo Tanzania ilizundua simu za smartphone za Oppo A96 na Oppo A76 kwenye soko la Tanzania baada ya kufanya vizuri kwa toleo lake la series A na reno series. Kulia ni Meneja Mkazi Oppo Tanzania Lin Ke.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...