Na Said Mwishehe, Michuzi TV
NCHINI Tanzania chini sekta ya kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi na ukweli ni kwamba sekta hiyo inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa huku robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania.
Kwa kukumbusha tu sekta hiyo ya Kilimo ina uhusiano mkubwa na sekta zisizo kuwa za kilimo kupitia uhusiano wa usafishaji kwenda kwenye usindikaji wa mazao ya kilimo, matumizi na uuzaji nchi za nje;Inatoa malighafi kwa viwanda na soko kwa bidhaa zilizotengenezwa.
Kubwa zaidi Tanzania inazalisha takribani asilimia 97 ya mahitaji yake ya chakula. Uzalishaji wa mazao ya chakula unatofautiana mwaka hadi mwaka kutegemea kiasi cha mvua kilichopatikana.
Maendeleo ya kilimo yamekuwa chini ya Serikali/fedha za umma kwa kipindi kirefu. Hata hivyo marekebisho ya uchumi kwa jumla yamekuwa na yanaendelea kuwa na matokeo ya muhimu kwenye sekta ya kilimo.
Marekebisho ya kiuchumi yamesababisha kufunguka sekta hiyo kwa uwekezaji binafsi katika uzalishaji na usindikaji , uagizaji pembejeo za kutoka nchi za nje na usambazaji na masoko ya kilimo. Serikali imebaki na kazi ya usimamizi na usaidizi wa umma na dhima ya uwezeshaji.
Umuhimu wa sekta ya Kilimo katika nchi yetu pamoja na mambo mengine ndio sekta iliyopewa nafasi kubwa na Watanzania ,asilimia kubwa ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo.Wapo wanaolima Kilimo kwa ajili ya mazao ya biashara na wapo wanaolima kwa ajili ya chakula.
Tunafahamu Kilimo hakimtupi mkulima,hivyo kila Kona ya nchi yetu kilimo kimepewa nafasi kubwa.Wakulima wanakifurahia Kilimo bila kujali changamoto wanazokumbana nazo, changamoto kwao wakati mwingine wanaigeuza kuwa fursa .Ni jambo la kawaida kumuona mkulima anatumia jembe la mkono na bado akafurahia kilimo.
Ni jambo la kawaida kwa mkulima kulima kilimo cha kisasa na mambo yakaenda vizuri.Kubwa kuliko yote Tanzania imejaaliwaa kuwa na aridhi yenye rotuba,kuna maji ya kutosha yanayoweza kutumika kwenye kilimo cha umwagiliaji.
Kwa kutambua kuwa kilimo kimeajiri maelfu ya Watanzania, Serikali imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha Kilimo kinaendelea kukuwa na kuwa na tija kwa wakulima na Watanzania kwa ujumla.Bajeti ya Serikali kwenye sekta ya Kilimo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Kama ambavyo tunafahamu kuhusu Kilimo na umuhimu wake Ilani ya CCM ya mwaka 2020 inaeleza kwa kina mipango na mikakati ya kuendeleza kilimo na kupitia Ilani hiyo inafafanua kuwa hata katika kukabiliana na umasikini kilimo ndio njia sahihi ya kuwaondoa Watanzania kwenye umasikini hasa umasikini wa kipato .Hivyo tunapozungumza Kilimo lazima tuelewe Kilimo kimebeba hatma ya Watanzania walio wengi.
Nikiri sekta ya Kilimo imegawanyika katika maeneo mengi tu,katika Makala haya nataka kuzungumzia umuhimu wa kuhifadhi Mbegu bora za asili, mbegu ambazo zinahimili hali ya hewa ya nchi yetu ya Tanzania, Mbegu za asili ambazo zinahimili mazingira yaliyoko.Kwa kifupi nataka kuzungumzia umuhimu wa kuwa na benki za Mbegu za jamii.
Tunafahamu kwa sasa kukua kwa teknolojia, tumeshuhudia Mataifa mbalimbali duniani yakijikita katika kuzalisha mbegu na kuzisambaza katika Mataifa mengine.Lakini kwa upande wangu naamini Tanzania bado tunao uwezo wa kuhifadhi mbegu zetu za asili kwenye benki za mbegu za jamii.Ninaposema benki sina maana ya zile benki za kutunza fedha bali nazungumza maeneo maalum yanayotumika kuhifadhi na kutunza mbegu.
Hivyo tunakuwa na benki za mbegu ambazo zitasaidia kupunguza ile changamoto ya wakulima kuhaha kutafuta Mbegu inapofika msimu wa kilimo.Benki hizi zinaweza kuanzishwa na mtu mmoja,kikundi au taasisi.Ukweli uliopo benki za mbegu zinapatikana katika maeneo mengi duniani na zimekuwepo kwa miaka mingi zikiwa na lengo la kuhifadhi,kurejesha ,kuimarisha na kuboresha mifumo ya mbegu ya ndani.
Nieleze kitu kidogo kuhusu benki ya mbegu, kwa hapa nchini kwetu Tanzania mwamko wa wanajamii katika kuanzisha na kusimamia benki za mbegu ni mdogo.Benki hizo zilikuwa zinapatikana katika maeneo machache ya Dodoma na Mbeya.Benki hizo zinafahamika kwa majina mengi,wapo wanaoziita benki za Jeni za Jamii, nyumba za mbegu za mbegu za wakulima,vibanda vya Mbegu,hifadhi ya Mbegu za Jamii,maktaba ya Mbegu na wengine huziita benki za mbegu za jamii.
Kwa wakulima ambao wanazo benki za mbegu za jamii huhifadhi Mbegu za mazao ya aina mbalimbali zikiwemo zile zinazolimwa kwa wingi,mfano mahindi,mpunga aina nyingine za mbegu.Pia wanahifadhi mbegu za mazao yanayolimwa kwa uchache kama vile Mtama na mazao ambayo walaji wameyatelekeza kama viazi vikuu.Mbegu hizo zinaweza kuhifadhiwa kwa kiasi kidogo au kikubwa kulingana na hitajio na upatikanaji wake.
Kwa kufafanua zaidi zipo hatua na mchakato wa kuanzisha na kusaidia benki za mbegu za jamii.Aidha kuanzisha na kuunga mkono benki ya mbegu ya jamii inahusisha htua kadhaa, hivyo ni muhimu kupitia mchakato huo bila kukimbilia na kuruhusu muda wa kutosha wa kuingiliana na wakulima.Kipaumbele kinapaswa kutolewa kwa kujenga uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuanzisha na kusimamia benki ya mbegu.
Miundombinu kwa ajili ya kuhifadhi Mbegu ije badae baada ya jamiii kuwa na uelewa wa kutosha na kuwa tayari kuanzisha na kusimamia benki husika.Pia kuwa na jengo nzuri peke yake kwa ajili ya benki ya mbegu haifai ikiwa wakulima hawana motisha na ujuzi wa kulitumia.
Ni vema tukafahamu kuwa kuna hatua kuu tisa katika kuanzisha na kuunga mkono benki ya mbegu.Baadhi ya hatua hizo ,ya kwanza ni uchambuzi wa hali halisi ya Mbegu, hatua hiyo inahusisha shughuli tatu; uchambuzi wa aina mbalimbali za mazao yanayolimwa na mwenendo wake, uchambuzi wa mifumo ya mbegu na uteuzi wa jamii na sehemu la kuanzisha benki za mbegu.
Aidha uchambuzi wa aina mbalimbali za mazao yanayolimwa n muelekeo wake , iko hivi uchambuzi huo ni muhimu kwa kuwa unasaidia jamii kuelewa aina za mazao yaliyoko mashambani na pia kujua kama mazao hayo yako eneo moja tu au yamenea kwenye jamii nzima .
Pia hujulisha mazao yale yanayolimwa kwa wingi na yale ambayo yanakaribia kutoweka au ambayo yameshatoweka .Zoezi hili linaweza kukamilishwa kwa kuwa na maonesho ya mbegu ili kusaidia kujua mahali zilipo Mbegu ambazo ni adimu na kukamilisha orodha ya mbegu zilizopo na taarifa zake ambazo huingizwa kwenye daftari la mbegu.Shughuli hiyo husaidia kutambua walinzi wa rasimali adimu na za kipee na kujenga uelewa kuwa watu wengi kuhusu umuhimu wa mbegu za mbegu.
Katika uchambuzi wa mifumo ya mbegu,hiyo ni mahususi katika kutambua mifumo ya mbegu iliyopo na michango yake katika kutosheleza hitajio la mbegu kwa wakulima.Kuhusu uchambuzi wa jamii na sehemu ya kuzalisha benki ya mbegu hapa ni vema ikafahamika sababu mbalimbali zinapaswa kuzingatiwa wakati wa kuchagua jamii au eneo la kuanzisha benki za mbegu za jamii.
Hapo utaangalia upatikanaji wa aina tofauti za mbegu kwenye jamii, uzalishaji wa mbegu wa kutosha kwa mahitaji ya jamii , upatikanaji wa mbegu nzuri na bora ,mfano uwepo wa maduka ya pembejeo yanayouza mbegu za asili,uwepo wa wakulima wanaobadilishana ,wanaotunza na kuchagua mbegu na uwepo wa soko lenye wigo mpana wa mbegu.
Pia uwepo ujuzi shirikishi wa jadi wa mbegu, maarifa ya kutosha ya kuchagua mbegu bora ,nia ya vijana katika Kilimo, Mazingira mazuri ya sera yanayounga mkono mbegu za asili ,eneo liwe linafikika kiurahisi kwa wana jamii walio wengi .Eneo la kuhifadhi mbegu linaweza kuwa ni jengo la mwana kikundi.
Hatua ya pili ni kuhamasisha na kuiandaa jamii, ,hii ni kulingana na uelewa wa hali halisi ya bioanuai ya kilimo ndani ,wakulima wanaweza kuanza kuhamasishwa kushiriki katika shughuli za benki ya mbegu.Vikundi vidogo vy wakulima vinaweza kuanzishwa ambavyo vitaainisha mazao muhimu na kukusanya mbegu kwa niaba ya jamii kisha kufuatilia uzalishaji wa mbegu zilizopotea ,zilizopo hatarini kupotea .
Kuzalisha mbegu ni shughuli ya vitendo na kiashiria kuwa walulima wamehamasika .Hiyo inaweza kupanuliwa baadae kwa wanachama wa benki y mbegu ambayo pia wanakusanya mbegu kwenye mitandao yao.
Akielezea zaidi hatua hizo Mratibua Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kilimo hai( TABIO) Abdallah Mkindi anasema hatua ya tatu ni kuchagua aina za mbegu kwa ajili ya kuhifadhi ambapo anaeleza benki za mbegu za jamii huwa na lengo la kutunza Mbegu za mazao muhimu."Baadhi wanasisitiza kutunza mbegu za mazao ya jadi yanayohusiana na utamaduni wa ndani.
"Wengine wanaweka kipaumbele cha kutambua ,kuzalisha na kusambaza mbegu ambazo zinauwezo wa kuhimili changamoto za magonjwa na mabadiliko ya tabianchi kama vile joto,ukame na mafuriko.Mbegu za asili na zile zilozoboreshwa zinaweza kuchaguliwa kwa ajili ya kutunza, ni muhimu kwa Wana jamii kushauriana kuhusu aina za mbegu ambazo wanapendekezwa zikiwekwe kwenye benki zao"anasema Mkindi.
Wakati hatua ya nne , Mkindi anasema ni kuchagua mbegu bora na safi .Kigezo muhinu katika Uchaguzi wa mbegu ni kupata sampuli na kuchagua ambazo hazina magonjwa, hiyo inawezekana kwa kuchagua kutoka kwenye maeneo mbalimbali ya shamba na kutoka kwenye mimea na mashuke bora mbalimbali.
"Epuka kuchagua mbegu kunta kutoka kwenye mimea iliyo pembezoni mwa shamba ili kuondoa uwezekano wa maingiliano ya chavua . Tahadhari ichukuliwe ili kuchagua mimea ambayo haina magonjwa.Ni vema mbegu zisafishwe kuanzia shambani ili kuondoa zile zenye magonjwa,magugu na wadudu.Magonjwa ya mbegu husababishwa na kuvu,bakteria na virusi.
"Magonjwa mengi y kuvu yanatokana na udongo na hutokea kwenye uso ( mabano sehemu ya juu) ya mbegu ambazo hudsbabisha kushindwa kuota au kuwa na miche yenye magonjwa.Umakini unapaswa kuzingatiwa wakati wa kukusanya/ kuchukua mbegu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa mikononi, vifaa vya kuvunia kama vile kisu au panga, na mifuko au vyombo vingine ni safi,amesema.
Aidha Mkindi anasema ni muhimu kuondoa sampuli yoyote ya mbegu ambayo ina dalili ya kuliwa na wadudu au ina magonjwa na kurudia zoezi hilo wakati wa kusafisha, kwa kuwa wadudu na magonjwa yanaweza kuongezeka wakati mbegu zimehifadhiwa.
Anasema ubora wa mbegu unatakiwa kufuatiliwa mara kwa mara kwa kufanya yafuatayo; kuchunguza kwa macho chombo kilichohifadhia mbegu, kuondoa kwa mkono mbegu zote au sehemu yake na kukagua kiwango cha unyevu,uwepo wa wadudu na magonjwa .Pia kufuatilia kiwango cha joto na unyevu kwenye vyombo vilivyohifadhia mbegu kwa kutumia kupima joto na unyevu .
Kwa mujibu wa Mkindi hatua ya tano ni kuweka miundombinu inayofaa ili kuweka mbegu katika hali ya usafi,afya na kuwa hai, miundombinu stahiki ni muhimu iwepo."Miundombinu hii inaweza kuwa ya kawaida mwanzoni lakini ikaaendelea kuboreshwa kulingana na wakati na hitajio.
"Miundombinu hiyo ni pamoja na rafu( shelfu au biliji kama inavyotambulika kwa wenyeji wa Mtwara) ,makabati ya mbao na chuma,mzani wa kupimia mbegu, kaushio la jua , vifaa vya kuhifadhia mbegu vyenye ujazo tofauti, kifaa cha kupangia madaraja ya mbegu ( CD grader), nyaraka za kutunzia kumbukumbu, ubao wa matangazo pamoja na kipima joto na unyevu,anafafanua.
Hatua ya Sita ni kuingia taarifa za mbegu kwenye daftari la kumbukumbu , ambapo anaeleza benki za mbegu za jamii sio tu kuwa ni sehemu ya kuhifadhia mbegu na vipando lakini pia ni sehemu ambayo ujuzi wa asili na taarifa husika kuhusu mbegu za asili zinaweza kupatikana."Hivyo ni muhimu wakulima wakafundishwa kuweka taarifa za mbegu kwenye benki.
"Taaarifa hizo ni jina la mbegu( la asili au la kisayansi) ,matumizi yake maalumu, hali ya Sasa ya upatikanaji wa mbegu hiyo , sifa za jumla za mbegu hizo ,mbinu za kulima mbegu hizo ,kiwango cha usambazaji wa kilimo chake, uwezo wake wa kuvumilia magonjwa, ukame,thamani ya lishe yake, matumizi mbalimbali ya mbegu hiyo,"anafafanua Mkindi.
Aidha rejesta za kuweka kumbumbu za mbegu ambazo zinahifadhiwa kwenye daftari zijulikanazo kama rejesta ambazo ni rejesta ya mbegu zilizokusanywa na hilo ni daftari la mbegu zote zilizokusanywa kutoka kwa wakulima na kuhifadhiwa katika benki za mbegu za jamii.
Wakati hatua ya saba ni Kuzihuisha mbegu kwa kuzipanda mara kwa mara ,ambapo kwa ujumla benki za mbegu za jamii zinakuwa na kiaisi kikubwa cha mbegu za asili na pia zinahifadhi kiasi kidogo cha mbegu zilizoboreshwa.Kulingana na upatikanaji wa rasilimali benki za mbegu hufanya zoezi la kuzipanda mbegu mara kwa mara ili kubakia kuwa hai na kubaki na ubora wake wa uotaji.
"Kwa aina za mbegu ambazo zinamahitaji , wanachama wa benki za mbegu za jamii wanaweza kutoa kipande cha ardhi kwa ajili ya kuzizalisha.Kwa aina ambazo zina soko kubwa ni rahisi kuamua kiasi kinachozalishwa kila mwaka kulingana na mahitaji ya wakulima."anasema Mkindi.
Anataja hatua ya Nane ni Kushirikiana habari ambapo anasema kushirikiana habari na uzoefu Kati ya mwanachama,wasio wanachama na wadau wengine ni jukumu jingine muhimu la benki za mbegu za jamii.Kushirikishana huku kunaweza kufanyika kwa njia ya kufanya maonesho ya mbegu.Pia inaweza kufanyika kwa kuandaa matukio ya misimu ambapo wakulima hubadilishana mbegu na maarifa yanayohusiana na mbegu.
Pia vikundi vya wakulima vinaweza kutenga baadhi ya siku za kutembelea mashamba ili kujionea aina mbalimbali za mbegu zinazopandwa, kutumia fursa za mikutano ya Kijiji na mingineyo katika kupashana habari zinazohusiana na benki za mbegu .
Hatua ya tisa; Kufanya Ufuatiliaji na kupima matokeo ambapo benki za mbegu za jamii zinatumia mbalimbali ili kuhakiku kuwa mbegu zinazohifadhiwa ni zile zenye ubora ambao hauna magonjwa, wadudu,magugu na uchafu.
Pia Ufuatiliaji wa shughuli za benki pamoja na kupima matokeo yake hufanywa na timu ya usimamizi iliyoundwa .Dhumuni ni kuangalia nyuma na kupima malengo yanafikiwa au laa, Ufuatiliaji wa kila mwaka unaweza kujulisha jinsi benki ya mbegu ya jamii yaliyoweza kusimamiwa vizuri, ambaye alichangia katika shughuli zake na ambaye hakuwa na mbegu.
Home
KILIMO
MAKALA
NI WAJIBU WA WATANZANIA KUWEKA MKAZO KATIKA KUHAMASISHA UWEPO WA BENKI ZA MBEGU ZA JAMII NDANI YA NCHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...