Na Mwandishi Wetu,Michuzi Tv

Katibu Mkuu wa chama cha Walimu Tanzania ,(CWT), Mwalimu Deus Seif akiwa mkoani Tabora amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuamua kuwapandisha madaraja mawili kwa Mserereko walimu zaidi ya elfu 50000 nchini.

Mwalimu Deus amesema hayo alipokuwa akizungumza na Walimu ambao ni Wanachama wa CWT Katika ziara yake katika mkoa wa Tabora  

Mwalimu Deus amesema Rais Samia Suluhu amefanya mambo makubwa kwa walimu na ndani ya mwaka mmoja ameamua kutupa zawadi ya kutupandisha madaraja walimu .

ametaja kuwa baada ya Mwaka 2016/2017 watumishi wa umma kupandishwa madaraja lakini kukatokea zoezi la uhakiki hivyo waliokua wamepewa barua hizo kusitishiwa upandaji wa madaraja Kwa walimu na watumishi wengine hivyo kwa kuwa CWT wana jukumu la kumtetea Mwalimu nchini waliamua kufuatilia suala hilo.

"CWT itaendelea kufuatilia stahiki zote zinazomhusu mwalimu na pia nawaomba walimu wawajibike wakati tukiendelea kudai haki zetu" Seif.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...