Na Janeth Raphael - Dodoma
Asilimia 11 ya wamiliki wa Shughuli za kiuchumi Tanzania bara wamekopa kiasi Cha shilingi trilioni 1.8 kutoka SACCOs, Benki, na Taasisi ndogo zae fedha.
Hayo yamezungumzwa leo na Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Dkt Seraphina Mgembe wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jensta Mhagama katika ofisi za MKURABITA Dodoma wakati akipokea taarifa ya utekelezaji kuanzia Novemba, 2004 Mpaka Februari 2022.
Dkt Mgembe amesema wafanyabiashara 74,147 wamesajiliwa kwa kupewa leseni za biashara pamoja na kusajiliwa kama walipa kodi kwa kupewa namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN)
"Zaidi ya Trilioni 8 zimekusanywa kutokana na ada za leseni za Biashara katika Halimashauri ambazo MKURABITA imefanya urasimishaji biashara kwa kutumia mfumo wa vituo jumuishi vya urasimishaji na uendelezaji biashara" - Amesema Dkt Mgembe.
Aidha Dkt Mgembe amebainisha kuwa wafanyabiashara waliopata mafunzo wamekopa zaidi ya shilingi Bilioni 9.38 kwa ajili ya kuongeza mitaji ya biashara zao na wananchi waliorasimisha maeneo yao wameongeza usalama na uhakika wa miliki za ardhi kwa kuwa maeneo hayo yamepimwa na kupewa hati miliki zinazotambulika kisheria.
Hata hivyo Dkt Mgembe amesema tija ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara imeongezeka kutokana na mafunzo mbalimbali yaliyotolewa na MKURABITA kwa kushirikiana na wadau, pia ushiriki wa Wanawake katika Shughuli za uzalishaji mali imeongezeka kutokana na Wanawake kuwezeshwa kumiliki rasilimali na biashara.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi vya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jensta Mhagama amesema ili rasilimali za wanyonge ziweze kurasimishwa vizuri ni lazima kuwe na rasilimali watu bila rasilimali watu hata urasilimishaji wa rasilimali nyingine utakuwa ni mgumu.
Usimamizi wa rasilimali zote Nchini iwe ni madini, ardhi, Fedha, Biashara, bahari na maji na kila kitu kilichopo ni lazima kuwe na rasilimali watu yenye kuendenda katika mienendo bora, yenye maadili inayozingatia sheria kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma na baadae rasilimali watu hiyo itatekelezwa majukumu yake na wajibu wake kwa wakati unaostahiki na kwa mbinu, uzoefu uliopo na ubobezi ambao rasilimali watu hiyo inayo rasilimali zote nyingine Nchini zitaweza kuchangia kiasi kikubwa sana katika maendeleo ya Taifa." - Amesema Mhagama
Hata hivyo Mhagama amesema MKURABITA wakiendelea kuenenda katika mienendo inayofaa na maadili mema na kuachana na tabia mbaya za rushwa, uzembe kazini, kutokuwajibika, kutokutekeleza majukumu yao vizuri watakuwa na mchango mkubwa zaidi wa kujenga Taifa na hasa katika eneo la kusaidia rasilimali za wanyonge zisipotee bure na ziweze kuchangia katika ustawi wa wananchi wa Tanzania.
" Lakini Kwa dhati nawapongeza si haba kazi mnayoifanya ni kubwa na ni kazi inayoonekana, inayopimika na ni kazi ambayo inatakiwa kujivunia kama Taifa." - Mhagama
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jensta Mhagama (MB) akizungumza. Kushoto ni Mratibu wa MKURABITA Dkt Seraphina Mgembe.Mratibu wa MKURABITA Dkt Seraphina Mgembe akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa MKURABITA kuanzia mwezi November 2004 Mpaka Februari 2022
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...