Na: Mwandishi Wetu – Shinyanga
Kikundi cha Wanawake cha Mwasele – B (KIWAMWA) kilichopo Mkoani Shinyanga wametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa mbalimbali kwa wanawake sambamba na kuonyesha juhudi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Taifa.
Pongezi hizo zimetolewa na wanakikundi hao wa KIWAMWA walipotembelewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kikundi hicho.
Akiwa katika mazungumzo na wanakikundi hao, Mheshimiwa Katambi alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeendelea kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika jamii sambamba na kutoa fursa mbalimbali za uwezeshwaji kiuchumi kwa kundi hilo ili waweze kuchangia katika ukuaji wa maendeleo ya Taifa.
“Kuanzishwa na kufanikiwa kwa kikundi hiki cha Mwasele (KIWAMWA) ni ishara tosha kuwa wanawake wataenda kuwezesha familia zao, kuanzisha ama kuboresha biashara zao pamoja na kuondoa umaskini katika jamii kwa kuleta maendeleo haraka, hivyo kukikundi kuwa mfano mzuri wa kuingwa na wengine,” alisema Katambi
Aidha, Mbunge huyo aliahidi kuendelea kutekeleza jukumu lake la kuwatumikia wananchi ili kuwaletea maendeleo na kuendelea kuboresha huduma mbalimbali.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikundi hicho cha Wanawake cha Mwasele – B (KIWAMWA), Bi. Anna Mwalongo alisema kuwa mwanamke katika jamii amekuwa akipambana na vita ya umaskini kuanzia katika ngazi ya familia hadi kijamii, hivyo kupitia vikundi vya kusaidiana kiuchumi vimekuwa ni chachu ya kuwezesha wanawake waweze kusukuma gurudumu la maendeleo.
“Tunazidi kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake anazofanya kwa ajili ya kuleta maendeleo katika nchi yetu na kwa wananchi kwa ujumla,” alisema.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na Wanachama wa Kikundi cha Wanawake cha Mwasele – B (KIWAMWA) alipotembelea Mkoani Shinyanga.
Sehemu ya Wanachama wa Kikundi cha Wanawake cha Mwasele – B (KIWAMWA) wakisikiliza maelezo ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (Mb) walipokutana nae kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
Mwanachama wa Kikundi cha Wanawake cha Mwasele – B (KIWAMWA) Bi. Magreth Manoni (kulia) akieleza jambo wakati wa mkutao huo. Kushoto ni atikati ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi (Mb). Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...