Na Mwandishi Wetu,Michuzi Tv
Jumatano Machi 8, 2022: Katika Kusherekea siku ya Wanawake Duniani 2022, Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited, kupitia kinywaji chake namba moja cha Konyagi imezindua chupa yenye chapa maalumu kwa lengo la kuwatambua wanawake 50 kwa michango mbalimbali katika Jamii.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Chapa ya Konyagi, Pamela Kikuli alisema wamezindua chupa hizo Zaidi ya 50,000 zenye ujazo wa ml 500 ambazo ni maalumu na zitakuwa na ishara ya mwanamke (mwanamke mzaramo) tofauti na ile yenye ishara ya mwanaume kama ilivyozoeleka.
“Kama namna ya kutambua mchango wa wanawake, tumeamua kuzindua chupa hii mpya ambazo zitauzwa kwa mwezi huu kwa bei ya Tsh 8,000 ambayo ni bei elekezi,” alisema.
Alitoa wito kwa wapenzi wa kinywaji cha Konyagi kuwatambua wanawake ambao wamekuwa na michango mbalimbali katika jamii na kuwanunulia chapa hiyo maalumu kwa ajili ya Siku ya Wanawake Duniani kama namna ya kuwafannya wathaminiwe.
Alisema tayari Konyagi imeshawatambua wanawake 50 ambao wamekuwa na michango mbalimbali katika jamii na wamekabidhiwa chapa hiyo maalumu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2022.
“Chapa hiyo maalumu itapatikana katika maeneo mbalimbali nchini katika mwezi huu na tunatoa wito kwa wateja wetu wachangamkie chapa hii malumu,” alisema meneja huyo huku akiwakumbusha watumiaji wa kinywaji hicho waepuke kunywa na kuendesha vyombo vya moto.
Aliongeza kuwa ishara tu ndio itabadilika ila ladha ya Konyagi itabaki vile . “Hatujabadilisha ladha ya Konyagi bali tunawatambua tu wanawake wakatu wa Siku ya Wanawake Duniani kwa kuweka ishara ya mwanamke kwa baadhi ya chupa,” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...