Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Njombe Betreace Malekela,ametoa wito kwa wanawake kupendana na kusemeana vizuri ili waweze kufanikiwa na kukuza uchumi wao.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na baadhi ya wanawake mjini Njombe walioukutana katika hafla fupi iliyofanyika katika ukiumbi wa Miriam ili kuhamasishana na kupeana faraja katika majukumu yao.

“Kila aliyempenda jirani yake amefanikiwa,msichongeane,msichukiane niwaombe mnapokuwepo kazini mpendane na utamani sana mwenzako apande katika nafasi.Ni vizuri sana kusemeana kwenye kazi naamini utafanikiwa”alisema Betreace Malekela

Iren Nyambo ni muunadaaji wa tukio hilo lililowakutanisha wanawake,amesema lengo kubwa ni kila mmoja kujifunza na kutengeneza mahusiano ili kuyafikia mafanikio.

“Tumekutana wawake wa aina tofauti wakiwemo wajasiriamlai na watumishi wengine kwenye makampuni na taasisi mbali mbali za serikali na zisizo za kiserikali kwa kuwa tukikaa pamoja na kujifunza tutafanya vitu vikubwa sana”alisema Iren Nyambo.

Sandra Msigwa ni mmoja wa washiriki wa tukio hilo la wanawake ambaye pia ameweza kutoa maada katika tukio hilo amesema mikusanyiko hiyo imekuwa ikileta manufaa makubwa kwao na kutoa wito wanawake kujiamini,kujipenda na kujijari.

“Ninaendelea kuhamasisha wanawake kujiamini,kujipenda na kujijari kwasababu mtu ukijiamini itakuwa rahisi sana kuchangamkia fursa”alisema Sandra.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe Betreace Malekela akitoa semina kwa wanawake walioshiriki hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Miriam mjini Njombe.
Baadhi ya wanawake waliokutana katika ukumbi wa Miriam wakimsikiliza mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...