Na Amiri Kilagalila,Njombe
JESHI la zimamoto na uokoaji mkoani Njombe kwa kushirikiana na wananchi mkoani humo wamefanikiwa kuokoa mwili wa mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50 kwenye maji ya mto ruhuji ambaye hajafahamika ni mkazi wa eneo gani mwili wake ukiwa umenasa kwenye mawe ya mto huo.
Aidha tukio hilo limetokea kwenye mto eneo la njiapanda ya barabara kuu ya kuingia mjini Njombe na njia ya panda ya barabara ya kutoka Njombe kwenda wilayani Makete.
Akizungumza mara baada ya askari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Njombe wakishirikiana na wananchi kufanikiwa kuutoa mwili wa mtu huyo,kaimu mkuu wa kikosi cha jeshi la zimamoto na uokoaji, Inspector Loth Madauda amesema.
“Mazingira ya eneo ni sehemu ya maporomoko ya maji amabpo alinasa chini ya mawe kwa hiyo inaonekana kama ni mtu aliyetoka kwenye mto mwingine kwa hiyo hatujui chanzo chake katokea wapi”alisema Loth
Vile vile Inspector Loth Madauda ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na maji yanayotiririka.
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Njombe wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyeokolewa kwenye mto ruhuji mjini Njombe.
Gari iliyobeba mwili wa mtu uliokolewa kwenye mto ikiondoka katika eneo la mto ruhuji.
Mwili uliokutwa kwenye maji mto ruhuji ukipakiwa kwenye gari ya polisi baada ya kuopolewa kwenye maji.
Maporomoko ya maji ya mto ruhuji mjini Njombe ulikookotwa mwili wa mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...