Na Jane Edward, Arusha
Naibu waziri wa Kilimo Antony Mavunde amewahakikishia watafiti kutoka Tari kuwa wizara ya kilimo itahakikisha inawajengea uwezo ili kuweza kuzalisha mbegu bunifu pamoja na kufanya tafiti zenye Tija katika kilimo cha mbogamboga,matunda na viungo.
Mavunde ameyasema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Arusha alipotembelea maeneo mbalimbali ya kilimo katika kutoa hamasa ya mabadiliko ya sekta ya kilimo kwa ujumla.
Ameongeza kuwa kwa sasa watafiti wanatakiwa kuangalia Dunia inataka nini kwa kuwa zao la ngano ni zao linalohitajika zaidi ambapo kwa Tanzania inatumia zaidi ya Bilioni 15 kwaajili ya kuagiza ngano nje na wataalamu wa Tafiti wapo .
"Lazima sasa Tari wanatakiwa kuboresha Utafiti wao wanaoufanya ili kuendana na kasi ya soko la dunia" Alisema Mavunde
Amesema kuwa Utafiti ndiyo moyo wa Kilimo ambapo kwa sasa mauzo katika eneo la mbogamboga na Matunda ni milioni 750usd na malengo ya serikali ifikapo mwaka 2030 Tanzania inatakiwa kuingiza Dolla Bilioni mbili na Tari wanakazi kubwa kuhakikisha malengo hayo yanatimia.
"Kazi ya Utafiti isikome na nitawakutanisha na watu wa Tasta ambao wanausika na mambo ya viungo ili mkae nao na kujua katika soko la nje nini kinahitajika ili kuendana na wakati wa sasa" Alisema Mavunde
Kwa upande wake meneja wa kituo cha utafiti Tari Tengeru Dr Mpoki Shimwela anasema kuwa jukumu lao katika Utafiti katika mbogamboga na matunda kwa sasa wanajikita katika uzalishaji bora wa matunda na mbogamboga huku akiwataka Watanzania kuja kuchukua mbegu katika eneo husika kwa kuwa bidhaa zao zimefanyiwa Utafiti wa kutosha na sio kununua mitaani.
Ameeleza kuwa wamejikita katika mbegu za zao la ndizi mshare ambapo kwa sasa kuna ugonjwa wa mnyauko kwenye mbegu hizo ambapo wanajikita katika kuhakikisha wanakabiliana nalo kwa kutoa mbegu bora ambazo hazitawapa wakulima changamoto.
Dr Philemon Mroso ni kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na ubunifu Tari Tanzania ambapo anasema Tari inajikita katika upatikanaji wa mbegu zaidi na kufanya tafiti na kutoa mbegu tani laki tatu ili kuendana na kasi ya soko kwa sasa.
Amebainisha kuwa maelekezo ya waziri ni ya kufanyiwa kazi kwa kuwa Tari ni kituo cha Utafiti ambacho kitasaidia kuendana na Azma ya serikali ya Rais Samia pamoja na wizara ya Kilimo kuwa wabunifu na kuleta mabadiliko chanya katika Taifa la Tanzania.
Dkt. Mpoki Shimwela meneja wa kituo cha utafiti TARI Akizungumzia kuhusiana na maelekezo ya Naibu waziri wa Kilimo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...