Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni (CCM) Mhe. Abbas Tarimba ametimiza ahadi yake ya kutoa msaada kwa Binti mwenye ulemavu, Loyce Peter aliyeomba msaada huo wakati wa maandalizi ya pambano la masumbwi kati ya Bondia Abdallah Pazi (Dullah Mbabe) dhidi ya Twaha Kassim Kiduku.

Akizungumza wakati akikabidhi Msaada huo wa Pikipiki aina ya ‘Boxer’ kwa Binti huyo, Mhe. Tarimba amesema alikutana na Loyce wakati wa maandalizi ya pambano hilo, Agosti, 2021. Amesema alitoa ahadi ya kununua Bajaji lakini kutokana na mahitaji ya Jimbo (Kinondoni) imeshindikana kununua Bajaji na kushauri kununua Pikipiki.

“Lengo ilikuwa kununua Bajaji lakini kutokana na mahitaji mengi ya Jimbo, niliomba mbele ya familia yao, bora tununue Pikipiki ili imsaidie yeye na familia yake kupata riziki ya kila siku”, amesema Mhe. Tarimba.

Kwa upande wa Binti huyo, Loyce Peter ameshukuru Mhe. Bunge wa Kinondoni kumpatia msaada huo aliomuahidia mwaka jana walipokutana katika Jimbo hilo.

“Mungu akubariki, akuongezee na pia usichoke kutusaidia sisi wenye uhitaji maalum, ukitoa japo kidogo, Mungu atakuzidishia kile ulichotoa. Mimi nishakuwa mwanao, umenisaidia mimi umesaidia wengi, mimi nitasadia wengine. Ahsante!”, ameeleza Loyce.

Naye, Mama Mzazi wa Loyce, Bi. Restuta Paulo Mbyalu amemshukuru Mbunge Tarimba kutimiza ahadi hiyo aliyowaahidi kuwapatia msaada huo. Pia amemuomba kusaidia wengine wenye uhitaji kama alivyosaidiwa yeye kwa Mtoto wake Loyce.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Haroud Maruma amempongeza Mbunge Tarimba kutimiza ahadi hiyo kwa Binti huyo mwenye ulemavu. Amesema amefanya jambo hilo la kiungwana na la ki Mungu.

“Nitoe rai kwa Viongozi, Wilaya ya Kinondoni bado watu wengi wana nahitaji, asiwe Mbunge pekee, bali wengine watoe misaada kwa Wananchi wenye mahitaji, kwa sababu jambo hili ni la kiungwa na la ki Mungu”, amesema Maruma.
 Mbunge wa Jimbo la Kinondoni (CCM) Mhe. Abbas Tarimba (wa kulia) akikabidhi Pikipiki kwa binti mwenye ulemavu, Loyce Peter. Mhe. Tarimba amekabidhi Pikipiki hiyo baada ya kutoa ahadi mwaka jana.
Mama Mzazi wa Loyce Peter akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Mtoto wake kukabidhiwa Pikipiki na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni (CCM), Mhe. Abbas Tarimba.
ulemavu, Loyce Peter (wa kushoto) akizungumza baada ya kukabidhiwa Pikipiki hiyo aliyoahidiwa na Mbunge wa Kinondoni (CCM) Mhe. Abbas Tarimba.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni (CCM) Mhe. Abbas Tarimba akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akikabidhi msaada wa Pikipiki kwa binti mwenye ulemavu, Loyce Peter, tukio la kukabidhi ahadi hiyo limefanyika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni.
Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Haroud Maruma akizungumza wakati Mbunge wa Jimbo hilo akikabidhi msaada wa Pikipiki kwa binti mwenye ulemavu, Loyce Peter.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...