Na Mwandishi wetu, Mbulu

MBUNGE wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, Yustina Rahhi amekabidhi msaada wa magodoro 30 kwa wafungwa waliopo gereza la Wilaya ya Mbulu, ambao wanaupungufu wa magodoro 50.

Akizungumza wakati akikabidhi magodoro hayo, Rahhi amesema magereza ni chuo cha mafunzo hivyo wafungwa nao wanapaswa kulala sehemu nzuri wakati wakitumikia adhabu zao.

Amesema japokuwa magereza ni watu wanaonekana kuwa ni wahalifu ila nao wanatakiwa kulala vizuri wakati wakitumikia adhabu zao kulingana na makosa waliyofanya awali.

Amesema awali aliwahi kujitolea za rangi kadhaa za kupaka gereza la wilaya ya Mbulu baada ya kuona changamoto ya kupauka kwa jengo hilo, akishirikiana na wadau wa maendeleo.

“Jamii inapaswa kujitoa na kusaidia taasisi mbalimbali zenye uhitaji ikiwemo hospitali, shule, vituo vya watoto yatima na wenye kuishi katika mazingira hatarishi,” amesema Rahhi.

Amesema ni vyema kutoa misaada kwenye taasisi hizo zenye mahitaji ya kibinadamu kama vile malazi bora, chakula na mavazi ili nao waweze kujisikia vyema kwenye maisha yao.

Mkuu wa magereza wa wilaya ya Mbulu, Alfonse Ezekiel Katunzi amemshukuru na kumpongeza mbunge huyo kwa kujitolea msaada wa magodoro 30 ya kulalia kwa wafungwa hao wa gereza la Mbulu.

Katinzi amesema kutokana na mbunge huyo kujitolea magodoro hayo 30 yatakuwa yamepunguza changamoto ya upungufu wa magodoro 50 yaliyokuwa awali hivyo yamebaki 20.

“Taasisi ya magereza ina mambo mengi ya kuwahudumia wafungwa waliopo ndani ikiwemo malazi, chakula, sare na mambo mengine hivyo tunashukuru kwa msaada huu,” amesema Katunzi.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...