Na Mary Margwe, Mbulu
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, Yustina Rahhi ( kulia mwenye gauni la bluu, amekabidhi msaada wa magodoro 30 kwa ajili ya wafungwa waliopo gereza la Wilaya ya Mbulu, ili kupunguza changamoto ya upungufu wa magodoro.
Akizungumza wakati akikabidhi magodoro hay oleo Jumamosi Machi 12, 2022 Rahhi amesema magereza ni chuo cha mafunzo hivyo wafungwa nao wanapaswa kulala sehemu nzuri wakati wakitumikia adhabu.
“ Kila mmoja katika nafasi yake tunapaswa kujitoa na kusaidia taasisi mbalimbali zenye uhitaji ikiwemo hospitali, shule, vituo vya watoto yatima na wenye kuishi katika mazingira hatarishi hasa kipindi hiki cha Kwaresma,” amesema Rahhi.
Amesema ni vyema kutoa misaada kwenye taasisi hizo zenye mahitaji ya kibinadamu kama vile malazi bora, chakula na mavazi ili nao waweze kujisikia vyema kwenye maisha yao.
Kwa upande wake, Mkuu wa magereza wilaya ya Mbulu, Alfonse Katunzi amemshukuru na kumpongeza mbunge huyo kwa kujitolea magodoro 30 kwa ajili ya wafungwa hao wa gereza la Mbulu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...