NA FARIDA SAID MOROGORO.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Morogoro kitengo cha Ufundi, wamekabidhiwa vitendea kazi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milion 180,ili  kukabiliana na upotevu wa maji, ambapo asilimia 39 ya maji yanayozalishwa hupotea bila kuwafikia walengwa na kusababisha hasara ya shilingi Milion 500 kwa kila mwezi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi hivyo ambavyo ni Pikipiki 30 na Gari moja Mkurugenzi wa  Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Morogoro Mhandisi Tamimu Katakweba amesema kupatikana kwa vitendea kazi hivyo kutarahisisha utendaji kazi wa mafundi wa mamlaka hiyo kuweza kufika kwa wakati eneo la tukio  pindi taarifa ya upotevu wa maji itakaporipotiwa.

Amesema  kuwa uzalishaji wa maji kwa mji wa Morogoro ni  wastani wa Lita za ujazo 34,000 kwa siku  huku  mahitaji kwa siku yakiwa ni  Lita za Ujazo 67,000 hivyo kufanya upungufu kufikia Lita za ujazo 33,000.

Aidha ameongeza kuwa Pamoja na upungufu huo bado asilimia 39 ya maji yanayozalishwa hupotea bila kuwafikia walengwa huku chanzo cha upotevu wa maji kikiwa ni  uchakavu wa Miundombinu sambamba na Uharibifu unaofanywa na baadhi ya watu hasa wanaoendesha shughuli za kibinadamu kwenye maeneo hayo yaliyopitiwa na miundombinu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi MORUWASA Prof.Romanus Ishengoma ameigiza Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Morogoro kudhibiti upotevu wa  maji ambayo husababishia mamlaka hasara kubwa kila mwezi, huku akisisitiza utunzaji na usimamizi mnzuri wa vifaa hivyo ili  viweze kufanya kazi iliyokusudiwa na sio kufanya shughili nyingine.

Nae Meneja EWURA kanda ya Mashariki Nyirabu Musira ameipongeza MURUWASA kwa hatua walioifikia ya ununzi ununuzi wa vifaa hivyo ambavyo vitawasaidia katika utendaji wao wa  kazi za kila siku kwa ufanisi wa hali ya juu.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...