Na Abdullatif Yunus -Michuzi Kagera.

Wakati Dunia Ikisherehekea Siku ya Wanawake ambayo huadhimishwa Machi 08 kila Mwaka, Wafanyakazi Wanawake kutoka Kiwanda cha Kahawa Tanica kilichopo Wametumia Sherehe hizo Kuwakumbuka Wasichana waliopo Shuleni.

Wanawake hao wakiongozwa na Meneja wa Kiwanda hicho Mhandisi Rodness Milton wamefika Shuleni Rugambwa na Kuzungumza na Wasichana kutoka Shule za Rugambwa, Kagemu na Kajumlo Sekondari lengo likiwa ni kuwakumbusha mambo mbalimbali yenye mustakabari wa maisha yao.

Akizungumza mara baada ya kongamano lililobeba mada tofauti, Mhandisi Rodness amesema lengo la kufika kwao Shuleni Rugambwa ni kutaka kuwatia Moyo Mabinti hao na kuwakumbusha kuwa kesho yao ipo mikononi mwao.

Miongoni mwa mada zilizotolewa katika Kongamano hilo ni pamoja na Mada iliyohusu Umuhimu wa Elimu kwa Mtoto wa Kike iliyowasilishwa na Mhandisi Rodnes ambayo kwa kiasi kikubwa ilijaa ushuhuda wa maisha aliyopitia hadi kufikia kuitwa Meneja wa Kiwanda cha Kahawa Tanica.

Mada nyingine zilizowasilishwa ni pamoja na Matumizi Sahihi ya Mtandao katika Elimu iliyotolewa na Rahel Didas, Faida za Kumtegemea Mungu katika Masomo na Maisha ikitolewa na Consesa Jackson na Masuala ya Afya na Hedhi Salama ikitolewa na Witness Milton, Mada ya Kuendeleza Vipaji ikitolewa na Irene Bitumbe.

kwa nafasi nyingine akina mama hao wa Tanica wametoa zawadi kama ishara ya kuwakumbuka Mabinti hao ambazo ni Maji ya Kunywa na Kahawa kutoka Tanica, pamoja na Taulo za kike ili kusaidia wakati wa hedhi.


Mhndisi Rodnes Milton akikabidhi Zawadi ya Maji ya Kunywa ikiwa ni miongoni mwa zawadi walizofika nazo Shuleni Rugambwa, zawadi nyingine ikiwa ni Taulo za kike na Kahawa ya Kunywa.

Mhandisi Rodness Milton Meneja wa Kiwanda cha Kahawa Tanica akizungumza na Mabinti wa Shule za Rugambwa, Kagemu na Kajumlo kupitia Mada alaiyowasilisha ya Umuhimu wa Elimu kwa Mtoto wa Kike
Mama Mary Kalikawe Mdau wa Utalii na Mkurugenzi wa Kiroyela Tours ni miongoni mwa akina mama waliombatana na Wanawake wafanyakazi wa Tanica ili kzungumza na Mabinti hao.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Bukoba Bwn. Chinchibera akizungumza na Wanafunzi wa Kike wa Shule za Rugambwa, Kagemu na Kajumlo kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...