na Janeth Raphael - Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka achukizwa na wazazi kutokuwa wakali kwa watoto wao ambao hawataki kwenda shule.
Mtaka ameyazungumza hayo wakati akiwa katika ziara ya kikazi, Mazingira katika kata ya Iyumbu mtaa wa Iyumbu Mkoani Dodoma ambapo amezungumza na wazazi pamoja na viongozi wa kata hiyo.
"Diwani endelea kuelimisha watu wako ni jambo la aibu tuko mjini hapa watoto hawaripoti shule, watakuwa vibarua mjini hapa, yapo mambo ni lazima tuseme hayawezi kujirudia katika kizazi chetu.
Sio jambo la kuchekesha mwanafunzi anakuja kuanza kidato Cha kwanza ni mjamzito, yuko darasa la tano ni mjamzito kwangu hapana ni lazima watoto waende shule" Amesema Mtaka.
Mtaka ametanabaisha kuwa yapo mambo ni lazima yasemwe kuwa hayawezi kujirudia katika kizazi kijacho kuwa na wazee ombaomba wa leo ni lazima tuseme iishie hapo.
" Sisi vijana wa leo tusije tukazeeka tukawa wazee wa kuomba omba yapo mambo lazima tuyaseme mapema, Kama huko nyuma watu walizoea kwenda mjini kuomba lazima tuanze kuzalisha jamii ambayo watoto wake wanapokuja kuwa watu wazima hawataomba omba mitaani hatuwezi kuwa na Mkoa ambao ikifika mwaka 2040 bado tuwe na omba omba hapana tunawaandaaje hawa watoto ili wasije kuwa hivyo?" Mtaka.
Aidha Mtaka amesema watoto wanaochezea shule Leo ndiyo omba omba wa keshokutwa,
"Hao omba omba ambao unaamin ukimpa hela unaenda mbinguni ni kwa sababu hujasoma nae, huenda ukakutana na mtu akakuambia huyu alikataa shule akiwa la pili na alikuwa na vituko huyu usimuone hapo amezeeka" - Mtaka.
Hata hivyo Mtaka amesisitiza kuwa wazazi wazungumze na watoto wao mapema kuhusu elimu kwa kuwa huko mbele wapo watu wanakuja wakiwa wazee hawana Bima wala kiinua mgongo ni lazima watoto, vijana wa leo waambiwe.
" Kwa hiyo mtendaji wale wote ambao hawajapeleka watoto wao shule beba wapeleke pale shule wasafishe vyoo vya Walimu na wanafunzi, wasafishe darasa la watoto wao ili wajue kwamba upo wajibu wa kumpeleka mtoto shule, sisi Serikali tumetimiza wajibu wetu kwani Rais asingejenga madarasa wananchi si wangelalamika? Sasa Serikali imejenga leta mtoto hutaki hakuna cha bure piga shoo moja Mtendaji watakuheshimu tena kabla ya mwezi mtukufu usije ukakwazwa piga mapema." Amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akizungumza na Wazazi, Walimu na Wananchi wa kata ya Iyumbu Mkoani Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...