Na Maandishi Wetu, Michuzi TV
WAIMBAJI wa Kanisa la Adventista Wasabato wapato 58 ambao wamehitimu mafunzo Maalum ya muziki katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wameshauriwa kufanya muziki ambao utakuwa na Matokeo mazuri kwa maendeleo ya Kanisa,kiroho na kijamii.
Ushauri huo umetolewa mwishoni mwa wiki Machi 12,2022 na Mgeni Rasmi kwenye mahafali TaSUBa ambaye ni Ofisa Tarafa wa Tarafa ya Mwambao Bagamoyo Dorice Mwakatobe, ambapo amesema licha ya wahitimu hao 58 kumaliza mafunzo hayo wanatakiwa kutumia mafunzo hayo kuleta matokeo chanya kwenye jamii.
Amewataka wahitimu kuwa mabalozi wazuri kule waendako ili wengine waweze kupata fursa kujiunga na TaSUBa na kuendeleza vipaji vyao.
Aidha Dorice ameshauri Chuo kuendelea kuwa wabunifu wa kuanzisha kozi mbalimbali ambazo zitawavutia watu wengi na kuwa na soko kwa sekta binafsi na za Serikali.
"Nawapongeza TaSUBa kwa kazi nzuri ya kutoa mafunzo na viongozi wa kanisa kutoa malezi kwa wahitimu hawa wakati wote walipokuwa hapa chuoni". Amesema Bi.Dorice.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye amewapongeza viongozi wa kanisa la Waadventista Wasabato kuungana na taasisi hiyo kwa kutoa ushirikiano wa kutosha hasa katika masuala ya muziki wa injili na imani pindi mafunzo yakiwa yanaendelea.
Dkt.Makoye amewataka wahitimu kuyafanyia kazi yale yote waliyojifunza ili waweze kuona faida ya hayo mafunzo."Wahitimu mkitoka hapa basi mkaoneshe hicho mlichokipata hapa waliobaki waone mabadiliko lakini pia muendelee kukifanyia kazi ili kiweze kukua na na hatimae kufikia lengo".
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu Kusini Mwa Tanzania(STUM) Mch.Mark Walwa Marekana amesema Kanisa la Waadventista Wasabato lipo na litaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na TaSUBa kwaajili ya kutengeneza kitu ambacho kitampendezesha mwenyezi mungu.
Ameiomba Taasisi ya TaSUBa kuhakikisha wanaendelea kuibua vipaji vya vijana wakitanzania na baadae nchi za jilani kutamani kujiunga na Chuo hicho cha Sanaa na kuweza kukitangaza Duniani kote.
Amesema kuna uwezekano mkubwa mmoja wa Botswana ataweza kujiunga na chuo hicho kwani taarifa hizo anazo hivyo TaSUBa watengeneze vopeperushi vya kutosha viweze kufika katika nchi hiyo ili nawengine waweze kujumuika na kujiunga na Taasisi hii". Amesema Mch.Marekana.
Mmoja wa wahitimu akisoma risala mbele ya mgeni rasmi amesema , pamoja na mafunzo kufanyika TaSUBa wahusika walifanya mafunzo kwa vitendo kwenye makanisa yao yale waliofundishwa TaSUBa.
Amesema kushiriki katika mafunzo hayo wamepata mtazamo tofauti wa namna ya kuendesha ibada ya nyimbo makanisani pamoja na kutambua falsafa ya muziki wa kanisa la Waadventista Wasabato.
"Kila aliyehudhuria masomo haya ya muziki amefungua mlango wa kujifunza muziki kama vile utunzi, piano, mitambo, falsafa, uimbaji na uimbishaji".
Mgeni rasmi Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mwambao Bagamoyo, Bi.Dorice Mwakatobe akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wakati wa mahafali ya wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mrefu kwa Wahitumu wa Kanisa la Adventista Wasabato,yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa),mkoani Pwani.
Raha ya kuhitimu mafunzo kupongezwa na maua kidogo ya kunogesha hitimisho
Wahitimu wakiwa na nyuso za furaha baada ya kukabidhiwa vyeti vyao
Mmoja wa Wahitimu mkongwe akipongezwa.
Baadhi ya wahitimu wakiwa kwenye mahafali ya wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mrefu kwa Kanisa la Adventista Wasabato katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) yaliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Aliyekuwa mgeni rasmi wa tukio hilo Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mwambao Bagamoyo, Bi.Dorice Mwakatobe akizungumza katika mahafali ya wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mrefu kwa Wahitimu wa Kanisa la Adventista Wasabato katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa),mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye akitoa neno la shukuruni na pongezi kwa Wahitimu wote wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mrefu kwa wahitimu wa Kanisa la Adventista Wasabato yaliyofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa),mjini Bagamoyo mkoani Pwani mwishoni mwa wiki
Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu Kusini Mwa Tanzania(STUM) Mch.Mark Walwa Marekana akizungumza mbele ya Wageni waalikwa na wahitimu wa Mafunzo maalumu ya Muziki ya muda mrefu ya Kanisa la Adventista Wasabato katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), yaliofanyika mwshoni mwa wiki mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Baadhi ya Viongozi waalikwa wa kanisa la Waadventista Wasabato wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
Baadhi ya Wahitimu wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea jukwaani wakati wakisubiri kukabidhiwa vyeti vyao vya uhitimu wa mafunzo maalumu ya Muziki ya Muda mrefu kwenye mahafali yao yaliyofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa),mjini Bagamoyo mkoani Pwani mwishoni mwa wiki
Baadhi ya Wahitimu wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea jukwaani wakati wakisubiri kukabidhiwa vyeti vyao vya uhitimu wa mafunzo maalumu ya Muziki ya Muda mrefu kwenye mahafali yao yaliyofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa),mjini Bagamoyo mkoani Pwani mwishoni mwa wiki
Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu Kusini Mwa Tanzania(STUM) Mch.Mark Walwa Marekana akimkabidhi cheti maalum kwa Mwanafunzi wa mafunzo maalum ya muziki ya Muda Mrefu,Rebbeca Bweye wakati wa Mahafali yao ndani ya chuo cha TaSUBa,Bagamoyo mkoani Pwani
Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu Kusini Mwa Tanzania(STUM) Mch.Mark Walwa Marekana akiwatambulisha na kuwapongeza baadhi ya akina Mama wenye umri mkubwa kuliko wengine wote katika Mahafali hayo lakini bado wana uwezo na umahiri mkubwa wa kuimba jukwaani nyimbo za kanisa,Wanaoshuhudia kushoto ni Viongozi wa dini kutoka nchini Botswana
Home
HABARI
WAIMBAJI ADVENTISTA WASABATO WASHAURIWA KUFANYA MUZIKI WENYE MAENDELEO KWA KANISA,TaSUBa WATOA NENO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...