Baada ya kufanya kung’ara katika mashindano ya Taliss-IST na Isamilo, muogeleaji anayekuja juu kwa kasi, Lorita Borega sasa amepania kufanya vyema katika mashindano ya klabu bingwa ya Taifa.

Mashindano ya klabu bingwa ya Taifa yamepangwa kufanyika Machi 26 na 27 kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Masaki.

Lorita(10) ambaye ni muogeleaji wa klabu ya FK Blue Marlins, kwa sasa yupo katika maandalizi ya mwisho kuelekea katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Chama Cha Kuogelea nchini (TSA).

Nyota huyo wa Tanzania alisema kuwa lengo lake kubwa ni kushinda medali na vikombe katika mashindano hayo ambayo yanashirikisha waogeleaji kutoka klabu mbalimbali.

Lorita pamoja pamoja na kuwa na umri mdogo, mpaka sasa ameweza kushinda jumla ya medali 26 na vikombe vinne. Kutokana na kufabya vizuri, TSA ilimchagua katika timu ya Taifa ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya kanda ya nne Afrika (CANA Zone 4).

Alisema kuwa anajua ugumu na umuhimu wa mashindano hayo, lakini maandalizi yake yamelenga kuleta matunda zaidi ikiwa pamoja na kuhimarisha muda wake (PBs) kuvunja rekodi.

Muogeleaji huyu atashindana katika vipengele nane ambavyo ni mita 100 na mita 50 katika staili ya freestyle, mita 100 na mita 50 (backstroke), mita 50 (butterfly), mita 100 na mita 50(Breaststroke), na mita 100 katika staili ya Individual Medley (IM).

“Ni mashindano muhimu sana ambapo hata waogeleaji Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanatakiwa kushiriki. Hivyo natarajia ushindani mkubwa kwani kila muogeleaji ana malengo kama yangu,,” alisema Lorita.

Kupita mashindano ya klabu bingwa, TSA uchagua waogeleaji ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia, mashindano ya Afrika (CANA), nashindano ya Kanda ya Tatu ya Africa (CANA ZONE 3), Mashindano ya Afrika kanda ya nne, mashindano ya vijana ya dunia, Jumuiya ya Madola na Olimpiki.

 

Muogeleaji chipukizi, Lorita Borega akichupa (dive)  katika mashindano ya hivi karibuni

Muogeleaji chipukizi, Lorita Borega akijiandaa kuingia kwenye bwawa la kuogelea kwa ajili ya kushindana katika mashindano ya hivi karibuni


Muogeleaji chipukizi, Lorita Borega akishindana katika mashindano ya hivi karibuni



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...