MWENENDO wa hali ya uchumi kwa mwaka wa Fedha 2021/2022 umeendelea kuwa mzuri na kuzidi kuimarika na kukua kwa asilimia 4.9 licha ya kuwepo kwa janga la UVIKO-19 huku uhimilivu wa deni la Taifa ukiendelea kubaki katika wigo mzuri pamoja na Serikali kuendelea kutoa fedha zilizoelekezwa katika sekta mbalimbali kwa mujibu wa bajeti.
Hayo yameelezwa leo jijini Arusha na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba wakati wa mkutano wa utekelezaji wa Mkakati wa Mawasiliano wa Wizara ya Fedha na Mipango uliowakutanisha Wahariri na waandishi wa habari na kueleza kuwa uchumi umeendelea kuimarika na kukua na sekta nyingi.
Tutuba alisema kuwa katika utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2021/2022 hadi sasa, hatua mbalimbali za utekelezaji zimefanywa kwa mafanikio makubwa na mwenendo wa hali ya uchumi umeendelea kuwa imara.
Alisema kwa mujibu wa taarifa ya Bajeti iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba hivi karibuni imeeleza mpango wa Serikali katika kusimamia uchumi wa Nchi na hadi kufikia mwezi Februari imekwishatoa fedha za miradi zipatazo trilioni 8.4 zilizoelekezwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Aliitaja baadhi ya mradi hiyo mikubwa iliwemo reli ya SGR, matengenezo ya ndege na ujenzi wa viwanja vya ndege katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya ambayo ujenzi wake unaendelea kwa kasi.
‘’Pia, Serikali imeendelea kulipa mishahara kwa wakati, tangu Serikali ya Awamu ya Sita ilipoingia madarakani imejiwekea utaratibu wa kulipa mishahara kila ifikapo tarehe 23 kila mwezi.’’ Alisema Bw. Tutuba.
Akieleza kuhusu mwenendo wa deni la Taifa, Tutuba alisema kuwa, Serikali imekuwa ikilipa deni hilo kila tarehe ambayo imepangwa kwa utaratibu wa upokeaji wa fedha hizo za mkopo na kwa wakati na wameendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia makusanyo ya ndani, fedha za nje na katika mfuko wa Serikali.
Akifafanua kuhusu mfumuko wa bei, Tutuba alisema, Serikali imeendelea kusimamia na kuwezesha bei za bidhaa na huduma zisipande sana pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya kuzuia mfumuko huo licha ya duniani kukumbwa na janga la UVIKO-19 na sasa vita ya Urusi na Ukraine ila hali ya mfumuko wa bei umeendelea kusalia chini ya asilimia tano kama ilivyopangwa mpango katika wa maendeleo wa miaka mitano na kubainishwa katika bajeti ya 2021/2022.
‘’Hadi kufikia mwezi Februari mfumuko wa bei ulishuka hadi kufikia asilimia 3.7 kutoka 4.0 ya mwezi Januari…Hali ya uchumi inakuwa na mfumuko wa bei unazidi kuwa chini, hali ya maisha inazidi kuwa nzuri kwa wananchi.’’ Alisema Bw. Tutuba
Aidha alisema kuwa kwa mwezi Februari kuna akiba ya fedha za kigeni zipatazo trilioni 6.1 zinazoweza kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje kwa miezi 6.4 na kuvuka lengo la Umoja wa Afrika Mashariki iliyopendekeza nchi kuwa na akiba ya miezi minne.
Mkutano huo utakwenda sambamba na utolewaji wa taarifa ya mafanikio ya wizara ya Fedha katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais qa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakayotolewa Mkoani Arusha na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Arusha leo Jumatatu Machi 14, 2022. Kulia ni Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Perfect Kilenzo, Mwenyekiti wa Wahariri Bw. Ben Mwang'onda na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madeni Bw. Nuru Ndile pamoja na Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Jaustine .
Mkuu wa Kitengo cha Mwasiliano ya Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, akizungumza wakati wa kuikaribisha Meza kuu pamoja na Wahariri na Waandishi wa Habari wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Arusha leo Jumatatu Machi 14, 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel akisalimiana na baadhi ya Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Arusha leo Jumatatu Machi 14, 2022 kwa ajili ya ufunguzi wa Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madeni Bw. Nuru Ndile,Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Jaustine,Bw. Ben Mwang'onda ambaye ni Mwenyekiti wa Wahariri wa Warsha hiyo pamoja na Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Perfect Kilenzo
Home
HABARI
MWENDO WA HALI YA UCHUMI NCHINI UMEENDELEA KUIMARIKA,HUKU DENI LA TAIFA LIKENDELEA KUWA HIMILIVU - KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...