Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Wanawake wa Bodi ya
Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA, Irene Mutagaywa
amewataka wanafunzi walioko mashuleni kujikita katika kutengeneza
ndoto zao kwa kusoma kwa bidii ili kuwa sehemu ya wanawake waliofanikiwa
katika nyanja mbalimbali hapo baadaye.
Pia amesema mafanikio yoyote yanayoonekana hapa nchini na duniani kote kwa kiasi kikubwa pia yamechagizwa na uwepo wa wanawake huku pia akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa rais mwanamke wa kwanza hapa nchini Tanzania na pia kwa kuendelea kuwaamini wanawake katika nafasi mbalimbali za kiuongozi kwenye Serikali yake.
Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura. Kilikuwa ni chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadaye. Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina la Clara Zetkin. Yeye alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...