Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) inaendelea kuonyesha njia kwenye masuala ya kijinsia kwa kutoa fursa sawa kwa wanawake kwenye maeneo mbali mbali mbali kama ajira, elimu, mapinduzi ya kilimo
Napenda kusisitiza kuwa usawa siyo suala la wanawake, ni suala la kibiashara. Biashara yenye usawa ni biashara wezeshi. Usawa wa kijinsia ni muhimu kwa uchumi na jamii kuweza kusonga mbele,”alisema Mark Ocitti, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2022
Mkurugenzi huyo alisema kila mtu ana wajibu wa kusaidia kuwepo kwa usawa wa kijinsia. Wote tunawajibika kwa mawazo na matendo yetu kila siku. “Tukiamua kupinga ubaguzi wa kijinsia tunaweza na tukafurahia kwa pamoja mafanikio ya wanawake,”
Mark alisema SBL katika programu zake inahakikisha kuwa ujumuishi wa makundi mbali mbali unakwepo. Kwa mfano katika programu yetu ya ufadhili wa masomo ya kilimo inayojulikana kama Kilimo Viwanda ambayo tumefadhili wanafunzi 200 mpaka hivi sasa, tumehakikisha kuwa uwakilishi wa nusu kwa nusu kati ya wanaume na wanawake unakuwepo,” alisema
Anasema pia SBL inaendesha program ya STEM ambayo huwachukua kutoka vyuoni vijana wa kike wanaofanya vizuri katika fani za sayansi, teknalojia pamoja na hisabati na kuwapa fursa ya kujifunza kwa vitendo kwa muda wa mwaka mmoja katika viwanda vyake.
“Tangu tuanzishe programu hiii mwaka 2020, vijana wengi wa kile wameweza kupata fursa ya kujifunza kwa vitendo katika idara zetu mbali mbali. Lengo letu ni kuona mtoito wa kike anakuwa sehemu ya maendeleo y sayansi kwa kunufuaika moja kwa moja na fursa mbali mbali,” alisema.
Mark anasema SBL kupitia kampuni yake mama ya Diageo imekuwa ikihamasisha ujumuifu wa makundi mbali mbali katika shughuli zake ikilenga kuwa na uwakilishi wa nusu kwa nusu kati ya wanawake na wanaume kufikia mwaka 2030.
Baadhi ya wanawake ambao ni waajiriwa wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kiwanda cha Mwanza, wakiwa katika picha ya pamoja na wazee katika kituo cha Bukumbi mfupi baada ya kutoa misaada mbali mbali katika kituo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku y Kimataifa ya Wanawake Duniani..
Baadhi ya wanawake ambao ni waajiriwa wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kiwanda cha Moshi, wakiwa katika picha ya pamoja na wauguzi wa hospital ya KCMC muda mfupi baada ya kutoa msaada katika wodi ya akina mama ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yaSiku y Kimataifa ya Wanawake.
Baadhi ya wanawake ambao ni waajiriwa wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kiwanda cha Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na walezi wa kituo cha kutoa mafunzo stadi cha muda mfupi baada ya kutoa misaada katika kituo hicho ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Dunia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...