Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani na kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri Muungano wa Tanzania Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) imeweka wazi azimio la kufikia usawa wa asilimia 50 kwa 50 kwa watendaji wa benki hiyo.


Kauli hiyo imetolewa leo wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki na kuhudhuriwa na Mtendaji Mkuu Theobadi Sabi na Menejimenti yake sambamba na wafanyakazi wa Benko hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, Mtendaji Mkuu wa NBC Theobadi Sabi amesema asilimia 48 ya wafanyakazi katika benki hiyo ni wanawake.


Sabi amesema, lengo la NBC ni kufikia usawa katika nafasi za juu za uongozi ambapo kwa sasa ni asilimia 30-33 ua wanawake wana nafasi za juu za uongozi kwenye benki hiyo.


“Tunatambua kama taasisi kwamba suala la maendeleo ya wanawake lina faida moja kwa moja kibishara, tafiti zinaonesha kwamba taasisi zinazochukua hatua wanawake wanawwza kufanikiwa na zenyewe zimefanikiwa,”


“kauli mbiu ya mwaka huu ni Kuvunja upendeleo ambapo benki yetu imelenga kuweka usawa wa asilimia 50 kwa 50 na ukizingatia asilimia 48 ya wafanyakazi ni wanawake,”amesema Sabi


Sabi amesema, wametumia siku ya leo kuzungumza na wafanyakazi wote wa NBC kuhusu masuala mbalimbali ya usawa na kuzindua programu kwa ajili ya wanawake zitakazowawezesha kusimamia usawa katika nafasi za juu za uongozi.


Ameongeza kuwa, kwa mwaka 2021 wafanyakazi waliofanya vizuri katika benki yao ni wanawake sawa na asilimia 53 na wanaamini kuendelea kuwekeza kwenye maendeleo ya wanawake ni kuwekeza mafanikio ya kibiashara.


Naye Afisa Mwajiri wa Benki ya NBC .... amesema katika siku hii ya wanawake duniani Benki ya NBC imelenga kumuinua mwanamke kwa kuanzisha akaunti mbalimbali za wanawake za Kikundi na Johari zinazomuwezesha kuweka akiba na hazina makato.


Amesema, Mbali na hilo NBC imekuwa na ushiriki mkubwa wa masuala mbalimbali ya wanawake na watashiriki katika kuchangia timu ya Twiga Stars.
 Mtendaji Mkuu Theobadi Sabi akiwahudumia wafanyakazi wake wakati wa maadhimisho ya Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...