Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalumu Dkt Doroth Gwajima  amesema wanawake ni waaminifu na wanajitum katika shughuli za kijamii ila wamekuwa hawaaminiki.

Dkt Gwajima ameyasema hayo wakati wa utoaji wa tuzo za Viwanda vya wanawake wajasiriamali zilizofanyika Jana usiku katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Amesema, wanaume wanatakiwa kuwaamini wake zao na kuwapa fursa za  kujiajiri ili kuweza kusaidia familia na kuacha imani  potofu.

“Wanaume mmekuwa mnawahisi vibaya wake zenu, hamuwaruhusu kujishughulisha na fursa za maendeleo ili familia ipate watoto wazuri wenye kila mmoja kati ya baba na mama kusimama katika nafasi yake,” amesema Dkt Gwajima.

“Taifa letu linaendelea kupigania haki ya mwanamke na serikali inaendelea kuonesha jitihada katika suala hilo na kwakuwa Tanzania yetu ni nchi ya ukombozi basi tujikomboe ili tukaokoe na wengine,”

Ameongeza kuwa, kupitia Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu ameendelea kudumisha mashirikiano na mataifa mengine ambapo tumeshuhudia mikataba 37 ya kibiashara imesainiwa na nchi mbalimbali na fursa hizo za kiuchumi zitakuja kuwakomboa taifa la baadae.

Akizungumza kwa niana ya Mkurugenzu Mtendaji wa Benki ya NBC, Neema Rose Singo amesema Benki hiyo imeweza kutoa mafunzo kwa wanawake zaidi kupitia klabu za wafanyabishara Nchi nzima na takriban wanawake 6000 wamenufaika.

Amesema, benki ya NBC imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara wapatao 200 katika kipindi cha maenesho ya Viwanda kwa wanawake wajasiriamali kwa mwaka 2022.

“Tumetoa mafunzo kwa wanawake wafanyabiashara takribani 200, na tunaamini mafunzo haya yataongeza tija katika uendeshaji wa biashara zao katika kipindi kifupi kijacho,”amesema

Amesema, maonesho ya mwaka huu yamewawezesha kama taasisi ya kifedha kuonesha bidhaa na huduma zao kwa wafanyabishara  na katika kipindi kifupi wameweza kwa kiasi kikubwa kueneza na kuongeza uelewa wa akaunti zao ambazo ni maalumu kwa ajili ya wafanyabishara hususani wakina mama.

“Benki ya NBC ina huduma mbalimbali. Zinazowalenga wanawake wajasiriamali ikiwemo akaunti ya Johari ambayo ni maalumu kwa wakina mama ambao wanania ya kuweka akiba ya uwekezaji wa baadae wakati huo mmilili akipatiwa riba hadi kufikia asilimia 7 pamoja na mikopo bila ya dhamama,” amesema
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalumu Dkt Doroth Gwajima wakati wa  utoaji wa tuzo za Viwanda vya wanawake wajasiriamali zilizofanyika Jana usiku katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa NBC kitengo cha biashara, Elvis Ndunguru akitoa tuzo kwa moja ya washiriki waliofanya vizuri wakati wa utoaji wa tuzo za Viwanda vya wanawake wajasiriamali zilizofanyika Jana usiku katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...