Waziri Maji Jumaa H. Aweso amezitaka Mamlaka za maji nchini kukaa na wadaiwa sugu ili kwa pamoja wakubaliane namna ya kulipa kidogo kidogo madeni yao badala ya kuendelea kuwasitishia huduma hiyo.

Ameyasema hayo wakati ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea na kukagua miradi ya maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga unaotekelezwa Mamlaka ya maji safi na mazingira ( DAWASA.)

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt.Christina Ishengoma amesema mradi hiyo ya maji itaweza kumaliza tatizo lililokuwepo katika maeneo ya Chalinze na pembezoni hivyo kufikia lengo lililowekwa na Rais Samia Suluhu Hassan la kumtua mama ndoo kichwani.

Ameishukuru  DAWASA kwa kuweza kusimamia mradi wa Mlandizi-Chalinze-Mboga na kuweza kumalizika kwa wakati kwani kumalizika kwa mradi huo kunawapa fursa wananchi kuanza kutumia maji safi na salama.

Naye Waziri wa Maji Jumaa H. Aweso ameelekeza Mamlaka za maji kukaa na wananchi wenye madeni ili kuangalia ni namna gani wanaweza kuyalipa madeni yao bila kukatiwa maji.
 
" kwenye ziara kama hizi miaka ya nyuma Wizara ya maji ilikuwa inapata changamoto kubwa kutokana na kutotimiza majukumu yake ipasavyo ya kusimamia Mamlaka za maji lakini kutokana na ufanisi mkubwa wa DAWASA sasa Wizara hiyo inatembea kifua mbele."amesema Aweso

Pia Aweso amewata DAWASA na RUWASA kuanza kuwaunganishia wananchi maji na kuacha ubabaishaji kwa kusema vifaa havitoshelezi kwa sababu wanachokitaka wananchi ni maji tu 

Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Mradi wa Maji wa Ruvu Juu hadi Mboga ni Mradi unaenda kuondoa kero ya upatikanaji wa Maji katika maeneo ya Mlandizi, Chalinze na Mji Mdogo wa Mboga

 Luhemeja ameongeza kuwa Mradi huo umelaza mabomba ya inchi 12 kwa umbali wa Kilomita 59 kutoka mtambo ya Ruvu Juu hadi Chalinze, Mji wa Mboga.

Ameongeza kuwa  Shilingi Bilioni 18 zimetumika kwenye Miradi wa Maji wa Ruvu Juu mpaka Msoga .

"Kukamilika kwake itatua kero ya Maji kwa wananchi zaidi ya 122,000 wa maeneo hayo na itakuwa ndio suluhu la upatikanaji wa maji kwenye mji wa Chalinze, Pingo, Pera, Msoga, Bwilingu, Msata, Kihangaiko, na Ubenazimozi."amesema na kuongeza

"Maagizo ya Waziri wa Maji pamoja na Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji tumeyapokea na tunakwenda kuyatekeleza kwa asilimia mia moja alisema Luhemeja
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma, Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakikaribishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kwenye mtambo wa uzalishaji wa maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara kamati ya Bunge ya kilimo, mifugo na maji ya kutembelea mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma, Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa ndani ya mtambo wa uzalishaji wa maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara kamati ya Bunge ya kilimo, mifugo na maji ya kutembelea mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma, Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu uendeshaji wa pampu ya kusukumia maji ya Chamakweza wakati wa ziara kamati ya Bunge ya kilimo, mifugo na maji ya kutembelea mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga.

Ziara ikiendelea 
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma, Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu uendeshaji wa pampu ya kusukumia maji ya Mboga wakati wa ziara kamati ya Bunge ya kilimo, mifugo na maji ya kutembelea mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt.Christina Ishengoma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na maji ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga.
Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na maji ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na maji ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa Mlandizi Chalinze-Mboga uliogharimu sh. Bilioni 18 na kulaza Bomba kubwa za inchi 12 kwa Kilometa 59 mara baada ya kumalizika kwa wa ziara ya kamati ya Bunge ya kilimo, mifugo na maji ya kutembelea mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...