Na Jane Edward, Arusha

Kutokana na changamoto ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini, Serikali imeshauriwa kuelekeza nguvu katika kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo vinavyozalisha mafuta ya parachichi ili kufanya mafuta hayo kutumika kwaajili ya kupikia.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (COSTECH) Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Avomeru inayojihusisha na mafunzo na ubunifu ya kuchataka bidhaa za maparachichi (AVOMERU GROUP) Jesse Oljange amesema uhitaji wa bidhaa hizo ni mkubwa.

Amesema uhitaji wa maparachichi hasa katika viwanda ambavyo vinatumia bidhaa za parachichi kama Mali ghafi ni mkubwa hivyo Serikali inawajibu wa kuwekeza katika viwanda vinavyozalisha maparachichi kwa wingi ili kujiwekeza katika kuandaa mafuta ya kupikia na kupunguza uhaba wa mafuta hayo.

"Mafuta ya maparachichi ni mafuta ambayo ni salama na kuna uwezekano mkubwa wa mafuta haya kutumika kama mafuta ya chakula hasa kwa kipindi hiki ambacho watu wanalalamika kuhusu bei ya mafuta'Alisema Jesse.

Ameongeza kuwa uwepo wa Avomeru umesaidia wakulima wa parachichi kukuza vipato vyao ambapo kwa vikundi ambavyo wanasimamia wakulima hupata faida zaidi ya Milioni moja kwa mwaka tofauti na hapo awali.

Nao baadhi ya wakulima wa parachichi Pascal Shayo amekiri kuwepo kwa soko kubwa la parachichi lakini wakati mwingine ni changamoto ya ukame unaopelekea ukosefu wa maji.

Hata hivyo wakulima wadogo na wakati wametakiwa kuona Fursa hiyo na kuongeza uzalishaji na kutambua jamii ya maparachichi yanayohitajika katika soko la kimataifa hasa maparachichi jamii ya HASS na jamii ya FUERTE ambapo serikali ikijikita Kwenye uwekezaji wa zao hilo.

Moja kati ya vifaa vilivyopo katika kampuni ya Avomeru.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Avomeru Jesse Oljange akionyesha waandishi baadhi ya teknolojia za kukamulia Mafuta ya parachichi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...