WASANII wanawake wa Sanaa za ufundi na wa maonesho ya jukwaani, wameshiriki katika program ya Museum Arts Explosion (MAE) kwa Mwezi Machi kwa kuonesha umahiri wao katika Sanaa za Ufundi hasa uchoraji pamoja na Ngoma za asili, maigizo, sarakasi pamoja na Musiki wa asili.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho hayo, Raisi wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho nchini Bi Anjewele ambaye ndiye alikuwa Mgeni rasmi amesema, program hiyo ya MAE imekuwa msaada Mkubwa kwa wasanii nchini kwa kuwa inatoa nafasi kwao ya kufanya maonesho na kuonesha kazi za Sanaa bure.
“Programu hii kwetu sisi wasanii ni msaada mkubwa, inachochea hari kwa wasanii kuendelea kubuni na kufanya kazi za Sanaa maana changamoto kubwa tunayoipata ni mahala pa kuoneshea kazi zetu ili tukutane moja kwa moja na wapenzi wa kazi zetu, asante sana Makumbusho ya Taifa kwa programu hii”. Alisema Bi Anjewele
Akizungumzia program hiyo, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure amesema wameona MAE ya mwezi huu ibebe ujumbe unaho husu Nguvu ya Mwanamke kama sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na Mhe Rais wa Jamuuhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan za kuipeleka Tanzania katika maendeleo makubwa.
“Programu hii itaendelea kutoa nafasi kwa wasanii wetu, nitoe wito kwa wasanii wote nchini kutumia fursa hii ya kuonesha kazi zao za Sanaa kupitia MAE, hapa kuna fursa nyingi watazipata hasa za kukutana moja kwa moja na wateja wao badala ya kazi zao za Sanaa kupitia kwa madalali wasio waaminifu”. Aliongeza Bw Bufure
Naye Profesa Paula Uimonen kutoka nchini Sweden alieudhuria Maonesho hayo, amesema ni adimu kuona kazi nzuri kama zilizo oneshwa na wasanii hao wanawake, kwani licha ya kuburudika kazi hizo zimekuwa zikifundisha na kumjengea mtu uwezi wa kufikiri kwa kuwa Sanaa hizo zinahijafi ufikiri zaidi ili kupata maana.
Maonesho hayo ya Museum Art Explosion hufanyika kila ijumaa ya mwisho wa Mwezi kwa wasanii kuonesha Kazi za Ufundi na Jukwaani ambazo zimezingatia maadili ya mtanzania pamoja na utamaduni wetu, ambapo kwa mwezi huu Maonesho ya Sanaa za Ufundi yaliandaliwa kwa kushirikiana na SafinaNevi Events.
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania, Bi Cynthia Henjewele akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Maonesho ya Museum Arts Explosion, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania, Bi Cynthia Henjewele akifungua rasmi Maonesho ya Museum Arts Explosion, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.
Watu Mbalimbali wakiangalia kazi za Sanaa za ufundi kwenye Maonesho ya Museum Arts Explosion, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...