Na.Mwandishi wetu,Michuzi tv

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Ally Ngwando amesema siri ya ushindi wake ni kuzingatia maelekezo ya kocha wake.

Ngwando ameshinda kwa pointi kwa majaji wote watatu kwa alama 76, 77 na 78 baada ya kumchakaza vikali mpinzani wake, James Kibazange katika pambano la fainali ya Champion wa Kitaa lililofanyika jana katika Uwanja wa ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Pambano hilo la utangulizi la kuwania mkanda wa ubingwa wa PST wenye uzani wa kilo 51 raundi nane.

 ushindi huo utakuwa chachu ya kuongeza bidii katika mazoezi yake ili kufabya vema katika mapambano mengine.

Ameeleza kuwa  ndiyo mara yake ya kwanza kushinda mkanda tangu alipoanza kucheza ndondi.

"Sijamini pale muandaaji aliposema kuwa ataweka mkanda kati yangu na James nimwambia kocha nitahakikisha nashinda ili kuwapa furaha mashabiki na kujiwekea rekodi nzuri, " alisema Ngwando.

Amesema huo ni mwanzo tu atahakikisha anaongeza juhudi ya mazoezi mara mbili zaidi ili kuweka fiti.

Muandaji wa pambano hilo, Meja Selemani Semunyu amesema pambano la Champion wa Kitaa limekuwa na mashabiki wengi jambo ambalo hakudhani kuwa hivyo.

Ameeleza  lengo la shindano hilo ni kuibua vipaji vipya ambavyo vipo mtaani lakini havionekani kwasababu ya mabondia kukosa fursa.

"Huu ni mwanzo tu wa pambano la Champion wa Kitaa, tulifanya kwa udongo ila mashabiki watuheshimisha na kulifanya jambo hili kuwa kubwa, naamini mwakani mambo yatakuwa mazuri zaidi, " alisema Semunyu.

Semunyu amesema katika pambano hilo wamechagua mabondia watatu waliofanya vizuri kwa ajili ya kuonyesha burudani nzuri kwa wakazi wa Morogoro katika pambano la bondia Twaha Kassim 'Twaha Kiduku' dhidi ya Alex Kabangu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Katika mtanange huo pambano kubwa (main Card) lilikuwa kati ya bondia, Maoli Ally dhidi ya Salehe Mkelekwa, ambapo Maono alishinda kwa TKO.

Baadhi ya Mapambano mengine ni Said Mkola alishindwa kwa KO dhidi ya Hamad Mkunde, Selemani Galile alimchakaza vikali Musaa Dragon kwa TKO, Abdallah Pazi  maarufu kama Dullah Mbabe' alimpa onyo kali bondia, Amour Sheikh kwa kipigo cha KO.

Wengine ni Adam Mbenga alionyesha ubabe kwa kumpiga Hassan Ndonga KO pambano la raundi nane lilimalizika raundi nne.

Bondia Abdallah pazia maarufu kama "Dullah Mbabe" akitangazwa Mshindi mara baada ya kumpa onyo kali Bondia  Amour Sheikh Kwa kupigo cha KO pambano ambalo limefanyika katika ukumbi wa ndani wa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Bondia wa Ngumi za kulipwa nchini Ally Ngwando mara baada ya kukabidhiwa Mkanda wa ubingwa wenye uzani wa kilo 51 na Mratibu wa pambano hilo Meja Selemani Semunyu katika pambano la champion wa kitaa lililofanyika uwanja wa ndani wa  Taifa jijini Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...