*Walikata Bima NIC wanarudishiwa hasara ya unyaufu wa korosho

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Shirika la Bima la Taifa (NIC) limelipa shilingi milioni 46 kwa Kampuni 11 ambayo hununua mazao ya korosho Mkoani Lindi na Mtwara na ambayo yamekata Bima kutoka NIC kutokana na uharibifu wa mazao hayo.

Akizungumza na waandishi wa mara baada ya kukabidhi hundi kwa wafanyabiashara wa Korosho Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Yesaya Mwakifulefule amesema malipo ya Bima hizo ni kutokana na hasara iliyotokana na unyaufu wa mzigo koroshokuwa uliokua umehifadhiwa ktk maghala mbali mbali mikoani humo.

Mwakifulefule amesema kuwa NIC iko katika kuhakikisha wafanyabiashara na wakulima kupitia Bima ya Kilimo wanakuwa na na amani na uhakika wa mitaji yao pindi wanapofikwa na majanga na kufanya biashara iendelee kutokana na bima walizozikata kutoka NIC.

"Sisi ndiyo Bima tupo kwa ajili kutoa huduma bora kwa wateja pamoja na kufanya biashara kuwa endelevu na mitaji ikiwa salama kuendeleza kuwekeza maradufu katika sekta ya kilimo"amesema Mwakifulefule.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalani Sangye Bangu amesema kuwa taasisi zingine ziige kwa bima pamoja na kutoa huduma.

Amesema kuwa wafanyabiashara katika sekta ya korosho wananeemeka na NIC kwa kwa kurudishiwa hasara waliopata uchakavu.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Yesaya Mwakifulefule akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi za Kampuni 11 zinazonunua Korosho katika Mikoa ya Lindi na Mtwara baada ya korosho hizo kunyauka ,jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja Yesaya Mwakifulefule na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalan Sangye Bangu wakimukabidhi moja ya kampuni hundi mmoja wa kampuni zilizonunua Korosho baada hapo zikanyauka ambapo Bima inalipa kutokana na unyaufu huo jijino Dar es Salaam.

Mfanyabiashara wa Kampuni ya Amargo ,Amani Lila akizungumza baada ya kupata hundi kutoka NIC ,jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyabiashara wa kanpuni za kununua korosho Lindi na Mtwara wakisiliza mawasilisho ya watendaji wa NIC na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalani.jijini Dar es Salaam.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...