Na Fredy Mshiu
Kamati
ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na thamani ya fedha
katika utekelezaji wa miradi ya majisafi katika Jiji la Dar es salaam na
Mkoa wa Pwani.
Pongezi
hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kamati katika mradi wa maji Makongo
hadi Bagamoyo uliogharimu kiasi Cha sh. Bilioni 65 na kuonyesha
kuridhishwa na utekelezaji wa wake.
Kaimu
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge hesabu za Serikali Mh. Japhet
Hasunga (Mb) ameeleza lengo la ziara hiyo ililenga kukagua thamani ya
fedha zilizotolewa na kutekeleza katika miradi mbalimbali inayosimamiwa
na DAWASA.
"Sisi
kama kamati ya Bunge tumefanya ziara hii Ili kuona na kutathmini
thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali katika mradi mbalimbali, na
kwa niaba ya Kamati nikiri kuwa tumeridhishwa sana na kazi
zilizotekelezwa na DAWASA na kila mmoja wetu amejionea na kuridhika na
kiasi cha fedha kilichotumika kwenye miradi hii."ameeleza Mh.Hasunga
Aidha
Mh.Hasunga ameongeza kuwa pia lengo la ziara ilikuwa kuona namna bodi
ya wakurugenzi DAWASA inavyowajibika katika kusimamia miradi kwa
kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya Serikali.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali mstaafu
Davis Mwamunyange ameieleza kamati kuwa mojawapo ya siri yakufanikiwa
katika utekelezaji wa miradi ya maji ni kutokana na uongozi mzuri
uliopo na weledi mkubwa baina ya Menejimenti na watumishi.
"Tumepata
mafanikio hasa katika kusimamia miradi mbalimbali ikiwemo huu wa
kuanzia Makongo hadi Bagamoyo kutokana na kufuata sheria na taratibu
zilizopo zinazoongoza Mamlaka na mashirika ya Umma".ameleeza Jenerali
mstaafu Mwamunyange
"Tunafurahi
kuona Kamati imeridhika na kazi kubwa tunaiyofanya ya usimamizi wa
fedha na utekelezaji wa miradi kwa thamani halisi ya hela, hii inatutia
moyo sana na tunawaahidi uwajibikaji zaidi ili kufikia malengo
yaliyowekwa" ameongeza Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange.
Mradi
wa maji *Makongo hadi Bagamoyo* unatekelezwa kupitia fedha za wadau wa
maendeleo na kusimamiwa na DAWASA kwa gharama ya kiasi cha Tsh Bilioni
64. Mradi utakapokamilika utahudumiwa wakazi zaidi ya 450,000 wa maeneo
ya Changanyikeni,Vikawe, Goba, Bunju, Madale,
Wazo, Ocean Bay, Salasala na sehemu ya mji wa Bagamoyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...