Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI kongwe ya Ulinzi hapa nchini, SGA Security, wamepongezwa na Jeshi la Polisi kwa kuzingatia vigezo vya kitaaluma wanapoajiri walinzi and kuwapa mafunzo.

Pongezi hizo zimetolewa katika hafla ya kufuzu kwa askari 50 wa SGA waliomaliza mafunzo ya mwezi moja yaliyoandaliwa na kampuni hiyo na kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Hafla hiyo iliongozwa na Afisa Polisi Jamii Wilaya ya kipolisi ya Kinondoni ASP Jane Dotto akiongozana na Mkaguzi Polisi Jamii Wilaya ya Kinondoni Insp Samwel Mkama Monge.

Mahafali hayo ya wahitimu wa mafunzo ya Awali wa kampuni binafsi ya Ulinzi ya SGA ilioko Oysterbay na Ada estate Kinondoni yalifanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo, Mbezi Beach.

ASP Dotto, katika hotuba yake, alisisitiza kuhusu ushirikiano uliopo katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kusisitiza kuwa haiwezekani Askari wa kampuni binafsi anaona tukio likitokea mbele yake na kutokuchukua hatua akidhani sio jukumu lake.

“Mlezi wa makampuni binafsi ya Ulinzi ni Jeshi la Polisi hivyo tofauti iliyopo ni ndogo sana yatupasa tufanye kazi kwa pamoja kwa manufaa ya Umma.,”alisema.

Alisisitiza ushirikiano mwema kwenye mapambano haya uimarishwe na mafunzo waliyopata Askari hao yasiwe kwa manufaa ya kampuni tu bali yawe kwa jamii nzima kwa ujumla wake.

“SGA ni Kampuni inayotoa ushirikiano wa karibu sana kwa Jeshi la Polisi na inafanya iwe rahisi kwasaidia koboresho mifumo ya ueandeshaji”, alisema ASP Dotto.

Alisema SGA inafuata vigezo vyote vilivovyowekwa na Jeshi la Polisi wakati wanaajiri, ikiwemo kuchukua tu askari waliofuzu mafunzo ya kijeshi – Mgambo and JKT – , kuthibisha afya kupitia maafisa wa OSHA na kuthibisha kuwa hawana rekodi ya ualifuli kwenye kanzi data ya alama za vidole ya Jeshi hilo. “SGA pia wamekuwa mstari wa mbele kuomba msaada wa mafunzo wa kuwaandaa askari kwa kazi zao, jambo ambalo inaturahizisha kazi yetu kama Jeshi la Polisi”, aliongezea.

Meneja Rasilimali watu wa SGA, Ebenzer Kaale, alieleza kuwa siri ya mafanikio kwenye fani ya Ulinzi ni mafunzo ya weledi ya mara kwa mara kwa maofisa wote, ambao wanachaguliwa kwa kuzingatia vigezo maalum yaliyotolewa na Jeshi La Polisi.

“Tunathamini sana maafisa wetu na tunaipa kipaumbele uwezo wao wa kiutendaji kwa kuwapa maarifa wa kutosha na kuwapa motisha kufanya kulingana na matakwa ya wateja wetu”, alisema Kaale.

Kampani ya SGA inaajiri Watanzania 6,000 na inatoa huduma zake kote nchini, haswa ya walinzi wa kawaida, wa silaha, wa Mbwa, usafirishwaji wa vitu vya thamani, ufungaji wa mitambo ya ulinzi na huduma za dharura kama ambulensi na zima moto. Kampuni hiyo imeshinda tuzo sita kuu mwaka wa 2021, ikiwemo Kampuni bora ya Ulinzi nchini Tanzania na Afrika Mashiriki, na pia Kampuni bora kwenye mitambo ya kulinda migodi, ubora wa huduma, uzingatiaji wa utumiaji.
Afisa Polisi Jamii Wilaya ya kipolisi ya Kinondoni ASP Jane Dotto akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu.
Afisa Polisi Jamii Wilaya ya kipolisi ya Kinondoni ASP Jane Dotto akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...