Na. Damian Kunambi, Njombe

Katika kuadhimisha miaka 10 ya Shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Participatory Development Concern (PADECO)limeadhimisha miaka hiyo kwa kujumuika na watoto wenye Mahitaji maalum katika shule maalum Mundindi.

Akizungumza Katika maadhimisho hayo Mkurugezi wa shirika hilo Willbard Mwinuka amesema shirika hilo likiwa kama msimamizi wa mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana katika shule hiyo maalum kwa kushirikiana na uongozi wa shule limekabidhi bweni la wanafunzi wa kiume lenye thamani ya sh. Milioni 53, 236,000, vitanda vya juu na chini(Double decker) 25 pamoja na magodoro 50.

Sanjali na hayo pia wamekabidhi Pikipiki aina ya Honda yenye thamani ya sh. 3,800,000 pamoja na vifaa vitakavyowawezesha watoto hao kukaa kwenye pikipiki kwa usalama zaidi kama kiti na mwamvuli.

Mradi huu ni mwendelezo wa miradi mingine ambayo ilitangulia awali katika shule hiyo ambapo mwaka 2017 shirika la PADECO lilikabidhi bweni la wasichana ambapo mpaka sasa linaendele kutumika.

Aidha kwa upande wa Kaimu Mkurugezi wa Halmashauri ya Ludewa Gilbert Ngailo amelipongeza shirika hilo kwa kuendelea kuleta maendeleo katika wilaya hiyo ambapo licha ya mchango wao katika shule hiyo Maalum lakini pia wamekuwa wakichangia maendeleo katika maeneo mengine ya Elimu, Afya, Maji, Ujasiliamali, Mazingira na Nishati Mbadala.

Ameongeza kwa kuwaasa vijana wengine kuiga mfano wa shirika hilo ambalo linaongozwa na kijana mwenzao kwani amekuwa ni mtu wa kujitoa katika maendeleo kwa kutafuta wafadhili mbalimbali kutoka Ujerumani hivyo wao kama Halmashauri wameona ushiriki wake huo hivyo hawana budi kumuunga mkono.

Amos Mtitu ni Mkuu wa shule Maalum Mundindi amelishukuru shirika hilo na kusema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni hatua kubwa kwao kwani italeta chachu kwa wazazi wengine ambao wameacha watoto wao nyumbani kutokana na mabweni kutojitosheleza hivyo kwa sasa wanatarajia kupata wanafunzi wengi zaidi.

Mkurugezi wa shirika la PADECO, Willbard Mwinuka
Baadhi ya vitanda vilivyokabidhiwa katika shule maalum Mundindi kutoka kwa shirika la PADECO
Bweni jipya la wavulana lililosimamiwa nashirika la PADECO katika shule maalum Mundindi
Baadhi ya Wanafunzi wenye Mahitaji maalum wa shule maalum ya Mundindi
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...