Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli ameipongeza Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kuendelea kuibua vipaji vya vijana wa Kitanzania kupitia sanaa mbalimbali.

Bw.Kaziyareli alitoa pongezi hizo wakati akisoma hotuba kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika Mahafali ya wahitimu wa Mafunzo ya muda mfupi katika Chuo cha TaSUBa, ambao wamefadhiriwa na wafadhiri mbalimbali.

Amesema kuna umuhimu wa wahitimu kuhakikisha wanazitafuta fursa kupitia mafunzo waliyoyapata na wasisubiri fursa ziwafuate.

Nae Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye amesema kampuni ya TCC PLC imekuwa ikidhamini vijana kupata mafunzo ya sanaa katika Chuo hicho tokea mwaka 2017 na vijana hao wanahitimu wakiwa wamejengeka vyema kabisa.

“Wahitimu wanaohitimu leo ni Vijana waliofadhiriwa na Taasisi ya TULIA TRUST vijana 25 na wengine wamefadhiriwa na Kampuni ya MUSICIANS FOR A BETTER LIFE vijana wapatao 58”. Amesema Dkt.Makoye.

Aidha Dkt.Makoye amewataka wahitimu kuwa Mabalozi wazuri kwa wengine ambao watahitaji kujiunga na Chuo hicho ili nao waweze kukuza vipaji vyao.

Kwa upande wake mwakilishi wa Wahitimu wa mafunzo, akitoa risala mbele ya Mgeni rasmi, Martine Mwangomale amesema kupitia mafunzo walioyapata ya muda mfupi yamewasaidia kuongeza ujuzi na maarifa katika Sanaa ambayo wamekuwa wakiifanya, Pia wameweza kushirikiana na kubadilishana mawazo baina yao na Walimu waliokuwa wakiwafundisha Chuoni hapo.

Amesema muda wa kushiriki mafunzo hayo yalikuwa ni mafupi hivyo wameomba Kwa wakati mwingine mafunzo kama hayo yatolewa Kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.

Pamoja na hayo wamewashukuru walimu kwa kutoa ushirikiano wa kutosha tangu walipofika chuoni hapo na kuanza mafunzo, kwani ushirikiano walioupata umewajengea uelewa mkubwa kupitia mafunzo hayo.

“Tunamshukuru mama yetu Dkt.Tulia Ackson Mwansasu Kwa kutupatia fursa hii nzuri ya kuendeleza vipaji vyetu katika Sanaa”. Alisema Mwangomale.
Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli akizungumza katika mahafali ya Wahitimu wa mafuzo mafupi ya sanaa Chuoni TaSUBa, wakati wa Mahafali yaliyofanyika chuoni hapo,Bagamoyo mkoani Pwani

Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye akizungumza mbele ya Meza kuu na Wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi (hawapo pichani) Chuoni TaSUBa, wakati wa Mahafali yaliyofanyika chuoni hapo,Bagamoyo mkoani Pwani

Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Sanaa waliofadhiriwa na Shirika la MUSICIANS FOR A BETTER LIFE wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo

Mkurugenzi wa shirika la MUSICIANS FOR A BETTER LIFE kutoka nchini Ujerumani Prof Anne Buter akizungumza mbele ya Meza kuu na Wahitimu wa Mafunzo ya sanaa ya muda Mfupi (hawapo pichani) wakati wa Mahafali yaliyofanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Naibu Mkuu wa Chuo, Mipango fedha na Utawala Emmanuel Bwire akizungumza mbele ya Meza kuu na Wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi (hawapo pichani) Chuoni TaSUBa, wakati wa Mahafali yaliyofanyika chuoni hapo,Bagamoyo mkoani Pwani
Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli akimkabidhi cheti kwa mmoja wa Wahitimu wa mafunzo ya  Muda mfupi ya sanaa Chuoni TaSUBa, Mahafali hayo yamefanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye akifurahia jambo na mmoja wa wahitimu wa Mafunzo ya Sanaa ya Muda mfupi Jose George kutoka jijini Mbeya baada ya kukabidhiwa cheti chake cha kuhitimu na Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo Bw.Alidis Kaziyareli kwenye Mahafali yaliyofanyika TaSUBa mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
  Taasisi ya TULIA TRUST imewafadhiri vijana 25  kutoka jijini Mbeya kusoma TaSUBa na kihitimu mafunzo yao ya sanaa ya muda mfupi.

Meza kuu ikifuatilia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa jukwaani na Wahitimu.

Wanafunzi Wahitimu wa mafunzo ya Sanaa ya muda mfupi wapatao 25 waliofadhiriwa na Taasisi ya TULIA TRUST wakiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu.

Wanafunzi Wahitimu wa mafunzo ya Sanaa ya muda mfupi wapatao 58 waliofadhiriwa na shirika la MUSICIANS FOR A BETTER LIFE la nchini Ujeremani wakiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...