Janeth Raphael- MichuziTv. Dodoma

Ikiwa Dunia wiki hii imeadhinisha  kilele cha maadhimisho ya presha ya macho Duniani,Wananchi washauriwa kujitokeza kwa ajili ya kupima macho yao angalau Mara moja kwa Mwaka 

Hayo yameelezwa  na Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho Dkt Jacinta Feksi  kutoka hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma alipofanya mahojiano Maalumu na mwandishi wetu wa MichuziTv kutoka Dodoma

" Kauli mbinu ya ya presha ya macho ni  'Dunia ni angavu tunza uoni wako ' kwa kweli tumewaona watu wakitambua kuwa kweli dunia ni angavu na wamekuja kuangalia afya ya macho yao ili dunia yao kuwa angavu" - Dkt Jacinta

Dkt Jacinta amesema tangu wiki ya presha ya macho ianze Hospitali hiyo ya Benjamini Mkapa wamefanikiwa kuona takribani wagonjwa  250 ambao ni mwitikio mzuri  na kati yao wagonjwa 50 wamekutwa na presha ya macho ambao wataendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi kwa kuwa ni jambo endelevu.

Presha ya macho ni ugonjwa namba mbili duniani kwa kusababisha upofu na bahati mbaya huwa hauna dalili ni ugonjwa ambao ni mwizi wa taratibu wa uoni na haugingi hodi mwanzoni hauna dalili" - Dkt Jacinta

Aidha Dkt Jacinta amesema kuwa kadri dunia inavyosogea kuna matumizi ya simu, komputa na vitu ambavyo vinaletaa Mwanga katika macho unakuta watu wanakaa sehemu moja wakiwngalia kitu hicho hicho kwa muda mrefu kwa karibu hivyo inapelekea madhara makubwa ya macho kuadhirika.

Moja kati ya vihatarishi au visababishi vya ugonjwa wa presha ya macho ni kuwapata watu wenye umri zaidi ya miaka 40 pia watu ambao kwenye familia Kuna mtu anaumwa ugonjwa huo unaweza kurithishwa kwa watu wa karibu mfano Kama ni mama basi watoto wake wana hatari ya kuupata ugonjwa huo na watu ambao wana magonjwa ya presha, kisukari hivyo ni moja ya vihatarishi zaidi ya Kupata magonjwa hayo ya presha ya macho.

Dkt Jacinta amesema wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali hiyo Wana utaratib wa kuwafuatilia kujua afya zao Zaidi kwani Kuna siku Maalumu kwa wiki imetengwa kwa ajili ya baadhi ya magonjwa 

Hata hivyo Dkt Jacinta amesema changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa wagonjwa wanaotakiwa kufanyiwa  upasuaji wa macho mara nyingi wamekuwa hawataki kwa kuwa kule mtaani wanapoishi wanakuwa washajazwa maneno mengi na hivyo kupelekea kazi matibabu ya mgonjwa kuwa magumu.


Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma Dkt Jacinta Feksi akizungumza jambo na baadhi ya waginjwa wakiofika hospitalini hapo kupata matibabu ya ugonjwa wa presha ya macho.

Mwandishi wetu Janeth Raphael akifanyiwa uchunguzi wa afya ya macho yake na Daktari Bingwa wa magonjwa ya presha ya macho kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt Jacinta Feksi.

Dkt Jacinta akipokuwa akizungumza na maandishi wetu  Janeth Raphael jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...