Kutoka Dodoma

Katibu mkuu wizara ya fedha Bw.Emanuel Mpowa Tutuba leo Machi 24 amewashukuru Washirika wa Umoja wa Mataifa (United Nations) kwa kuendelea kuisaidia Tanzania kwenye jitihada mbalimbali za kupambana na umaskini

Hayo ameyazungumza kwenye hafla fupi ya ufunguzi wa mpango wa Maendeleo baina ya Serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa (United Nations) Jijini Dodoma.

Aidha Bw.Tutuba aliongeza kwa kusema kutokana na juhudi za Umoja wa Mataifa Tanzania imefikia kwenye uchumi wa kati ambao umeongezeka kwa asilimia 6.7 pia kunaongezeko la umri wa kuishi kutoka umri wa miaka wastan 50.8 mwaka 2000 hadi miaka 65.5 mwaka 2018.

"Pamoja na hayo mashirika haya ya Umoja wa Mataifa yametusaidia kwenye mpango wa Maendeleo wa miaka mitano sambamba na mpango wa Maendeleo wa Zanzibar kufikia mwaka 2050" amesema Tutuba.



 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...