*Yaahidi kuendelea kulea vijana na wanafunzi katika Tehama.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema imeondoa gharama za majaribio kwa wanafunzi katika bunifu za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kupata matokeo chanya yatakayosaidia ukuaji wa uchumi wa kidijiti.
Pia imesema hadi kufikia Februari 2022 watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu wameongezeka na kufikia million 35.2.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam jana na Mkurungezi Mtendaji TCRA, Dk. Jabir Bakari wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya haki za watumiaji Duniani.
Alisema tayari ameshafanya mazungumzo na Kampuni zote za simu kuwa wanafunzi watakaofanya bunifu zinazohusiana hizo kupitia mtandao wasitozwe gharama yoyote na wameafikiana hivyo ili wanafunzi wa chuo na msingi kuwavutia kufanya masuala ya kitehama na kuendelea kulelewa.
"Nimeshazungumza na kampuni za simu kuwa wanafunzi wasitozwe gharama yoyote lengo ni kupata matokeo chnya katika uchumi wa kidigitali"amesema Dk.Bakari
Dk.Bakari alisema sekta ya mawasiliano imekuwa ikitumika kuhudumia uchumi wa fedha ambapo sasa hivi unaweza kutumia kama benki inavyotembea ikiwemo kulipa kodi na tozo za serikali na ankala mbalimbali haya ni mafanikio katika sekta ya mawasiliano.
"Ukuaji huu umesaidia kupeleka uchumi mbele, ongezeko hilo linatoa picha kuwa watumiaji wa mtandao wa huduma za fedha wanakuwa siku hadi siku"alisema.
Alisema TCRA itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kulinda haki za walaji pamoja na kuandaa mazingira ili utumiaji wenye manufaa uweze kukua kwa haraka.
Naye Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji TCRA, John Daffa alisema TCRA walianza maadhimisho hayo kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya oMawasiliano kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbal katika sekta hiyo.
Alisema maadhimisho hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza na utaratibu huo utakuwa endelevu.
Hata hivyo maadhimisho hayo yameambatana na uzinduzi wa Klabu mbalimbli za kidigitali lengo likiwa ni kuwawezesha wanafunzi kufahamu matumizi sahihi ya mtandao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...