Na Mwandishi Wetu
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)kupitia Mhifadhi Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro Robert Mwangosi amesema wamejikita kwenye ufugaji wa nyuki kwa kuwa wana manzuki kubwa sana maeneo ya Msingisi ambayo inafanya vizuri kwenye ufugaji nyuki ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita wamevuna tani moja ya asali kutoka kwenye mizinga 82 tu.
Akielezea zaidi Mwangosi amesema Gairo inafanya vizuri katika suala zima la uzalishaji wa asali ,hata hivyo wamekua wakijikita katika kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu ufugaji wa nyuki.
"Asali ya Fairo inasomeka vizuri katika soko ,imekua na sifa tofauti kwani asali yetu ina sifa ya kuganda kutoka na mimea ya maeneo hayo na mimea tunayoendelea kuipanda kwani tuna mimea inayoitwa Akeshia yale maua yake ndo yanayopelekea asali hiyo kuganda,"amesema.
Pia ubora wa asali ni mzuri na hiyo imefanya asali hiyo hununuliwa na watu wa nje ya Gairo na ndo mana wanaendelea kujikita katika kuwahamasisha wananchi kupanda miti na kuangalia aina ya mimea ambayo inafanya vizuri na inayo pendwa na nyuki na kuweza kufanya vizuri katika uzalishaji wa nyuki.
Kwa upande wake Ofisa Ufugaji Nyuki TFS Gairo Aled Heneriko ameeleza katika msimu huu wa mvua ni msimu wa nyuki kujenga hivyo ameshauri kwa wakati huu mizinga ambayo ilikua ina uchafu isafishwe ili wakati ambao makundi ya nyuki yanapokuwa yanahama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine yaweze kuingia katika hiyo mizinga kwaajili ya kujipatia mazao mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...