Na.Khadija Seif,Michuzi TV

KATIKA Kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Taasisi na Makampuni wamesisitizwa kuwakumbuka watoto wa kike Mashuleni na kuwapa Elimu ya hedhi salama Ili kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuendelea kuzalishwa kwa viongozi mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Taulo za kike katika Shule ya Sekondari Ben Bella iliyopo wilaya ya Magharibi kisiwani Zanzibar Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Salma yusuph amesema wakati wanawake wanaendelea kumsherehekea Mwanamke ni vyema kukajengeka nguzo imara kuanzia Kwa Mabinti na kuhakikishia wanakuwa kwenye Afya Bora na usalama pamoja na kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo Afya zao na kuhakikisha wanapata Hedhi Salama.

Hata hivyo ameongeza kuwa kutoa zawadi hiyo katika shule ya "Ben Bella" ni Muendelezo katika Kuiadhimisha siku hiyo ya kipekee Kwa Wanawake na wataendelea kuonyesha upendo huo katika Matawi mbalimbali nchini ikiwemo Arusha,Mtwara ,Dodoma na hata hivyo tayari wamekabidhi box kadhaa wa Kwa wanafunzi wa shule ya Pius iliyopo Kongowe jijini Dar es salaam.

"Ili awe kiongozi tunaemtaka ni lazima kufanyike jitihada za kuona Kwa jinsi gani Binti alieko shule anakuwa na Afya Bora hususani anapata Hedhi Salama na kupitia Majukumu yetu ya kibima kuhakikisha usalama wa wali ni matumaini yetu hivyo hivyo Kwa wanafunzi wetu tunawahakikisha hedhi iliyo salama kabisa."

Aidha Kwa upande wake Afisa Biashara na uwekezaji LuLu Mohamed amewasihi wanafunzi hao kuwa na nidhamu Ili waweze kufikia na kutimiza ndoto zao na kuwataka kuendelea kusoma Kwa bidii kwani yeye ni Mmoja wa zao la shule ya "Ben Bella" na hatimae Kwa Sasa ameshika nafasi kubwa Serikalini.

"Viongozi waongoza nchi hii wengi ni Wanawake hata mimi Nina nafasi kubwa na chimbuko lake ni hapa shule ya Ben Bella nimesoma hapa na hatimae nilifauli vizuri Masoko yangu hivyo mjitahidi kusoma Kwa bidii Ili muweze kuwa alama nzuri Kwa Shuleni yenu na Taifa Kwa ujumla."

Nae Mwalimu Msaidizi wa shule hiyo alitoa bi.Mwaminza amepongezi za dhati Kwa uongozi wa Shirika hilo kuwapa kipaumbele wanafunzi wa shule hiyo kupatiwa taulo hizo za kujikinga wawapo katika siku zao.

''tunashukuru Kwa zawadi hizi na zimefika muda sahihi kabisa uhitaji Kwa hapa shuleni ulikua ni mkubwa Kwa Mabinti zetu hivyo kipekee tunawashukuru na tumepokea zawadi hizi ."

Afisa Idara ya Elimu Mandalizi na Msingi Asha Haji
akikabidhi box la taulo za Kike Kwa Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Ben Bella iliyopo wilaya ya Magharibi kisiwani Zanzibar

Afisa Biashara na uwekezaji wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) Lulu Mohamed akizungumza na wanafunzi wa shule ya Secondary Ben Bella iliyopo wilaya ya Magharibi kisiwani Zanzibar mara baada ya kukabidhi taulo za kike kama sehemu ya Kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Ben Bella Sekondari Bi.Mwaminza akitoa neno la shukrani Kwa uongozi wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) Kwa kuchagua shule hiyo kama sehemu ya kuwakumbuka wanafunzi hasa Mabinti na kuwapatia taulo za Kike.


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ben Bella iliyopo wilaya ya Magharibi kisiwani Zanzibar wakiwa na taulo za kike walizopatiwa na Shirika la Bima Zanzibar ( ZIC) kama sehemu ya kusherehekea siku ya wanawake duniani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...